IQNA

Jinai za Israel

Utawala wa Israel umebomoa misikiti 56 katika vita dhidi ya Gaza

21:24 - November 07, 2023
Habari ID: 3477855
AL-QUDS (IQNA) – Utawala wa Kizayuni wa Israel hadi sasa umeshambulia na kuharibu kabisa kwa mabomu misikiti 56 tokea unazish vita vya maangamizi ya umati dhidi ya Ukanda wa Gaza. Aidha misikiti mingine zaidi ya 192 imepata hasara kwa kuharibiwa katika mashambulizi hayo ya kinyama.

Vyombo vya habari vya Gaza vinaripoti kuwa mashambulizi yanayoendelea ya utawala wa kivita dhidi ya Ukanda wa Gaza yamesababisha uharibifu mkubwa katika eneo lililozingirwa la Palestina.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Gaza, Salama Marouf, tathmini ya uharibifu huo ni pamoja na uharibifu wa miundo MSINGI mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maeneo ya ibada, vituo vya matibabu, taasisi za elimu na makazi ya raia..

Mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7 yamepelekea zaidi ya watu 10,000 kupoteza maisha wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Mashambulizi hayo yamewafanya watu milioni 1.5 kuyahama makazi yao, na kusukuma hali katika eneo lililozingirwa la Palestina kuwa janga la kibinadamu.

Mashambulizi ya utawala haramu wa Israel yalianza baada ya wapigania ukombozi wa Palestina wakiongozwa na harakati ya Hamas kuanzisha operesheni ya kushtukiza ambayo haijawahi kushuhudiwa dhidi ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu mnamo Oktoba 7, na kuua walowezi wa Kizayuni na wanajeshi zaidi ya 1,400 na kuwachukua wengine 200 mateka. Operesheni hiyo ya Hamas ilikuwa ni jibu kwa jinai za utawala haramu wa Israel ambao uliteka na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina mwaka 1948 chini ya himaya ya Uingereza.

Habari zinazohusiana
captcha