IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

Afisa wa zamani wa Jihad ya Kiislamu: Wapalestina wana azma ya kutetea ardhi yao

20:32 - November 04, 2023
Habari ID: 3477837
Al-QUDS (IQNA) - Kiongozi mkuu wa zamani wa harakati ya Jihad Islami (Jihadi ya Kiislamu) ya Palestina amesisitiza kuhusu azma ya taifa la Palestina kutetea ardhi yao inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Akizungumza katika mahojiano na IQNA, Omar Abdullah Shallah ameashiria hali ya Ukanda wa Gaza na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu baada ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya Oktoba 7 na kusema eneo hilo limebadilika kimsingi tangu operesheni hiyo ya kushtukiza iliyotekelezwa na harakati ya kupigania ukombozi wa Palestina ya Hamas.

Amesema operesheni hiyo ilisambaratisha sura ghushi ya kutoshindwa utawala wa Israel na hivi sasa serikali ambazo zimeanzisha uhusiano wa kawaida na Israel au zinatafakari kufanya hivyo zinapaswa kufikiria upya uamuzi wao huo na kusimama na wale wote wanaoiunga mkono Palestina.

Akikariri kuwa watu wa Palestina hawatakubali kuhamishwa na watapigana kulinda ardhi yao, Shallah alisema licha ya ukatili wote wa Israel katika Ukanda wa Gaza na uharibifu wa nyumba na miundombinu katika eneo la pwani, hakuna mtu anayezungumza juu ya kuondoka Gaza.

Mapambano ya kupigiani ukombozi wa Palestina yamekuwa katika makabiliano na wavamizi kwa takriban miaka 100 na kuongeza kuwa tangu vita vya mwaka 1967 utawala wa Kizayuni haujapata ushindi wowote bali umeshindwa katika vita na makabiliano yote.

Kwa neema ya Mwenyezi Mungu, haijalishi ni nchi ngapi zinakuja kuunga mkono utawala wa Israel katika majaribio yake ya kung'oa kuangamiza makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina, kwani hazitaweza kufanikiwa, alisema.

Akinukuu Aya ya 10 ya Surah Al-Ahzab katika Qur'ani Tukufu isemayo , “Walipo kujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu; na macho yalipo kodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali,” alisema Mtume Mtukufu (SAW). akaanza kuwalingania watu kwenye Uislamu, makundi yote yakaanza kumpinga na kukabiliana naye lakini Mungu akailinda dini na kuiletea ushindi.

Leo pia, Mwenyezi Mungu ataokoa makundi ya kupigania ukombozi wa Wapalestina dhidi ya Wazayuni na waungaji mkono wao, alisema.

Ameonya kuwa iwapo nchi za kieneo zitashindwa kuoanisha misimamo yao na matakwa ya watu wao wanaoiunga mkono Palestina, zitakuwa katika hasara.

Shallal amewataka wananchi wa eneo la Asia Magharibi kuendelea kutoa mashinikizo kwa watawala wao ili wapiganie kukomesha jinai za Israel dhidi ya taifa la Palestina.

Kwingineko katika matamshi yake, afisa huyo wa zamani wa Jihad ya Kiislamu amepongeza uungaji mkono wa Palestina kutoka kwa harakati za muqawama  au mapambano ya Kiislamu katika nchi nyingine, zikiwemo Yemen, Iraq, na hasa Hizbullah ya Lebanon, akisema inaonesha kuwa mhimili wa muqawama uko hai na hautaiacha Palestina.

Utawala wa Israel na waungaji mkono wake katika eneo na kwingineko wametambua sasa kwamba watu wa Gaza na Palestina hawako peke yao, aliendelea kusema.

3485861

Habari zinazohusiana
captcha