IQNA

Jinai za Israel

Marekani: Waandamanaji wanaounga mkono Palestina wasali nje ya ubalozi wa Israel

12:44 - December 02, 2023
Habari ID: 3477973
OTTAWA (IQNA) - Zaidi ya waandamanaji 100 Waislamu walikusanyika karibu na ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Marekani siku ya Ijumaa na kusali sala ya Ijumaa hapo sambamba na kulaani mashambulizi yanayoendelea ya utawala haramu wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji hao ambao walistahimili mvua, walipeperusha bendera za Palestina na kushikilia mabango ya kulaani uvamizi wa kijeshi wa Israel dhidi ya Gaza. Walitoa wito wa kukomeshwa kwa kuzingirwa kwa Gaza. Baadhi ya mabango yalisomeka: "Komesha mauaji ya kimbari", "Nasimama na Gaza" na "Komesha uhalifu wa Israel".

Baada ya Sala, waandamanaji walitoa nara kama vile "Palestine Huru, Huru", "Komesha kuzingirwa Gaza sasa" na "Sitisha mapigano sasa". Pia wameitaka serikali ya Marekani kusitisha usaidizi wake wa kifedha na kijeshi kwa Israel.

Maandamano hayo yalienda sambamba na kusambaratika kwa mapatano ya wiki moja ya usitishaji vita kati ya utawala wa Israel na Hamas siku ya Ijumaa.

Utawala haramu wa Israel ulianza tena vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza kwa mashambalizi ya anga dhidi ya eneo hilo.

Wizara ya Afya ya Gaza ilitangaza mwishoni mwa Ijumaa kwamba Wapalestina wasiopungua 178 wameuawa na 589 wamejeruhiwa tangu Israel kuanza tena kampeni yay a mauaji ya kimbari Gaza.

3486247

Habari zinazohusiana
captcha