IQNA

Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa ilivunja uti wa mgongo wa Israel

19:23 - November 24, 2023
Habari ID: 3477938
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Harakati ya Kiislamu (Muqawama) ya Kupigania Ukombozi wa Palestina (HAMAS) ilivunja mgongo wa Israel kwa kutegemea imani na ushujaa katika operesheni ya kimbunga ya Al-Aqswa.

Hujjatul Islam wal Muslimin Shekhe Kazem Seddiqi amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Sala ya Ijumaa mjini Tehran na kueleza kwamba, Wazayuni walitaka kuiangamiza Hamas, lakini wameshindwa katika matukio yote.

Akiashiria matukio ya hivi karibunii kabisa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amesema, Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa ndio yale malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kwani hakuna kinachoweza kufanywa dhidi ya mchokozi na mnyang'anyi kwa kujadilian na kufanya mazungumzo.

Ayatullah Seddiqi ameongeza kuwa: Katika miaka 44 iliyopita ya Intifadha ya Palestina, wananchi wa Palestina walikuwa katika hatua na nafasi ya kujihami, lakini safari hii wamekuwa katika nafasi ya kushambulia na watu waliofunzwa na kulelewa katika shule ya imani, jihadi na subira, katika siku moja na nusu, walifanikiwa kumtandika adui Mzayuni kwa kipigo cha knockout.

Akizungumzia mpasuko mkubwa uliopo ndani ya utawala haramu wa Israel, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran: Wazayuni wanaona uchungu sana kutokana na kutwishwa na kulazimika kukubali usitishaji vita, baada ya jinai na mauaji ya watoto, wanawake na wagonjwa. Kadhalika amesema, mashambulio ya harakati za muqawama Iraq, Yemen na Lebanon yanaonyesha kuwa, uti wa mgongo wa Wazayuni umevunjwa chini ya moto mkali wa muqawama.

4183792

Habari zinazohusiana
captcha