IQNA

Watetezi wa Palestina

IUMS Inatoa Wito kwa Siku ya Kimataifa ya Usaidizi kwa Gaza, Al-Aqsa

13:32 - December 07, 2023
Habari ID: 3478000
DOHA – IQNA: Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) umetoa wito wa kufanyika maandamano na mikutano kote duniani Ijumaa hii kuunga mkono Wapalestina wanakandamizwa Gaza na Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) sambamba na kulaani utawala wa dhalimu wa Israel.

Muungano huo ulihimiza Ijumaa, Desemba 8, iitwe siku ya kuunga mkono Ukanda wa Gaza na kuulinda Msikiti wa Al-Aqsa.
Aidha imetoa wito kwa mataifa ya Kiislamu na watu wanaopenda uhuru duniani kusimama kidete katika mshikamano na taifa la Palestina.
Zaidi ya Wapalestina 16,000 wameuawa na utawala wa Israel huko Gaza tangu ulipoanzisha mashambulizi yake mabaya kwenye eneo la pwani Oktoba 7.
Takriban miezi miwili baada ya mashambulizi ya umwagaji damu ya Israel, utawala huo ghasibu unafanya uharibifu katika kila kona ya ardhi, na kuacha njia ya vifo na uharibifu pia ukikata mojawapo ya maeneo yenye wakazi wengi zaidi duniani kutoka na vifaa vya msingi kama vile maji, umeme. dawa, na mafuta na kuacha mamilioni ya Wapalestina katika hatari ya njaa.
Wakati huo huo, ukiukaji wa utakatifu wa Msikiti wa Al-Aqsa unaendelea kufanywa na vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel na walowezi wa Kizayuyni.

4186340

Habari zinazohusiana
captcha