Lijue Shirika
la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)
Shirika la
Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) ndio la kwanza na la pekee ambalo
linashughulikia kwa njia maalumu habari za Quran katika ulimwengu wa
Kiislamu. Shirika hili lilianzishwa Novemba 11, 2003 sambamba na tarehe 11 ya
Mwezi Aban (Kalenda ya Hijria Shamsia) sawa na tarehe 15 ya Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani mwaka 1424 Hijria Qamaria katika sherehe iliyohudhuriwa na rais wa
wakati huo wa Iran.
Shirika hili lilianza
kwa habari 7 kwa siku kwa lugha ya Kifarsi na baada ya kupita miaka 15 ya kazi,
shirika hili sasa, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, linazalisha takribani habari
850 kwa siku kwa lugha 19 duniani ambapo hadi sasa habari zinazohusiana na
Qur'ani zilizoandikwa zimepindukia milioni moja na laki tatu.
Kwa
kuzingatia anuai ya lugha na ujumbe wa kimataifa wa IQNA, shirika hili mwezi
Machi mwaka 2013 lilipata kibali cha Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa
Kiislamu Iran na kubadilisha jina kutoka Shirika la Habari la Qur’ani la Iran
na kuwa Shirika la Habari za Qur'ani
la Kimataifa (IQNA) ili kwa njia hiyo, sawa na Qur'ani Tukufu, liweze kuwa
kiunganishi cha Waislamu kote duniani.
Malengo:
Malengo muhimu
yanayozingatiwa na Shirika la Habari la Qur'ani la Iran IQNA ni kama
ifuatavyo:
·
Kupasha haraka habari kamili kuhusu harakati na shughuli zinazohusiana na
Qur’ani Tukufu nchini Iran na duniani kote.
·
Kuakisi mazingira ya Qur'ani Tukufu yanayotawala katika Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran na nchi nyinginezo za Kiislamu duniani.
·
Kuhimiza jamii ilelekee katika mtindo wa maisha kwa msingi wa Qur’an Tukufu
·
Kujitahidi kuhakikisha kuwa mafundisho ya Qur’ani Tukufu yanatumika kama
mhimili mkuu katika sekta mbali mbali
·
Kuwabainishia Waislamu duniani kuhusu harakati za Qur'ani katika
mfumo mtakatifu wa Jamhuri ya Kiislamu
Lugha za
IQNA:
Shirika la Habari za
Qur'ani la Kimataifa (IQNA)hivi sasa linatayarisha habari za Qur'ani kwa
lugha 19 hai za dunia zikiwemo: Kifarsi, Kiarabu, Kiswahili, Kiingereza,
Kifaransa, Kiurdu, Kitaliano, Kichina, Kirussia, Kihispania, Kibengali, Kihausa,
Kipashtu, Kihindi, Kituruki, Kiazari na Kimalayu, Kifilipino na Kijerumani.
Matawi ya IQNA:
Ili kufanikiwa IQNA
katika katika kila kona ya dunia,
shirika hili la habari za Qur'ani limeanzisha matawi mikoani nchini Iran na
katika nchi za kigeni. Hivi sasa kuna matawi ya IQNA katika mikoa 30 ya Iran
na pia katika nchi sita duniani ifuatavyo.
1. Matawi ya IQNA mikoani
ni kama ifuatayo:
Ilam, Azerbaijan Magharibi, Azerbaijan Mashariki,
Ardabil, Alborz, Isfahan, Bushehr, Sistan na Baluchistan, Chehar Mahal na
Bakhtiari, Khuzestan, Khorassan Razawi, Khorassan Kaskazini, Kermanshah,
Gilan, Fars, Mazandaran, Markazi, Hormozgan, Hamedan na Yazd.
2.Maeneo ya kigeni
Eneo la Magharibi mwa Asia
Eneo la Mashariki mwa Asia
Eneo la Asia ya Kati
Eneo la Ulaya
Eneo la Afrika
Eneo la Amerika
Huduma za Habari:
Kutokana na kuwa lengo
la IQNA ni kueneza utamaduni wa Qur'ani katika nyanja mbali mbali za kidini,
kisiasa, kisanaa, kijamii, kiuchumi nk, katika kuanzisha idara na vitengo
vyake vya habari, IQNA imezingatia mahitajio ya wasomaji na udharura uliopo
katika kubainisha ufahamu wa Qur'ani Tukufu. IQNA inazingatia yafuatayo
katika kuanzisha vitengo idara zake kuu: A. Matuko: Hapa matukio yanajumuisha
kupasha habari kuhusu yaliyojiri katika setka au nyanja mbali mbali na
B.Maudhui. Idara hiihufuatilia maudhui mbali mbali za Qur'ani kwa kuzingatia
mahitaji ya wasomaji wa kila eneo na sera jumla za IQNA. Maudhui za Qur'ani
katika IQNA hutegemea ushauri wa wasomi na wataalamu ambao hufanyiwa
mahojiano na kisha waliyoyasema kuchapishwa katika jarida maalumu la kidijitali.
IQNA hivi sasa ina
vitengo 8 asili na vitengo vingine 64 vidogo vya habari ifuatavyo.
1. Harakati za Qur'ani
(Harakati za Qur'ani, taasisi za Qur'ani za wananchi, shakhsia na waandishi
habari wa kujitolea).
2. Siasa na Uchumi (Siasa
na Uchumi)
3. Maarifa ya kidini ( Hapa
wahusika ni wasomi na wanafikra wa
vyuo vya kidini au Hawza na vyuo vikuu)
4. Kijamii (jamii, afya na
mitandao ya intaneti)
5. Sanaa na Fasihi (sanaa,
fasihi, jihadi na hamasa)
6. Kimataifa (Kifarsi,
Kiarabu, Kiingereza, Kiswahili, Kirussi na lugha nyinginezo)
7. Mikoa
8. Media anuai na picha.
Kitengo cha waandishi
habari wa kujitolea wa IQNA, kilianzishwa mwaka 2003 kwa lengo la kuwa na
waandishi habari ambao wanajitolea kukidhi mahitaji ya kila siku ya habari za
Qur'ani kote nchini Iran. Kundi hili hivi sasa lina waandishi habari 7,268
waliojiandikisha ambapo 5,300 kati yao hutuma habari mara kwa mara. Kwa
wastani kitengo hiki hupokea habari 120.
Shirika
la Habari za Qura'ni la Kimataifa (IQNA) mbali na mipango na malengo hayo yaliyoainishwa pia linafuatilia na
kutekeleza mipango ifuatayo.
·
Kuandaa vikao vya kitaalamu
·
Kuchapisha jarida la "Rayhe” (Harufu Nzuri)
·
Kuandaa na kushiriki katika makongamano ya Qur'ani Tukufu
|