IQNA

Ramadhani Palestina

Azma ya Wapalestina wa Gaza kutekeleza ibada za Ramadhani hata baada ya Israel kubomoa misikiti

22:15 - March 10, 2024
Habari ID: 3478485
IQNA - Waislamu wa Palestina huko Gaza wamebakia imara katika Imani na hivyo wana azma ya kutekeleza ibada zote za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kukusanyika katika mabaki ya misikiti iliyoharibiwa na mabomu ya utawala haramu wa Israel.

Licha ya zaidi ya misikiti 1,000 kuharibiwa na kuwa magofu tangu Oktoba 7 kutokana na mashambulizi ya maangamizi ya umati yanayotekelezwa na utawala wa kidhalimu wa Israel kwenye eneo la Gaza lililozingirwa, waumini wanaendelea kufuata Uislamu kwa Imani thabiti isiyotikisika.

Msikiti wa al-Faruq mjini Rafah ulioanzishwa mwaka 1952 na kubomolewa hivi majuzi katika shambulio la anga Israel, umekuwa nembo ya subira na uvumilivu.

Wakati mmoja jengo kuu la msikiti huo liliokuwa na ukumbu wa swala wenye uwezo wa kukaribisha waumini zaidi ya 1,500 na maktaba kubwa sasa linatumika kama eneo  kukusanyika waumini pamoja na kuwa katikati ya uharibifu mkubwa.

Mwezi mtukufu wa Ramadhani unapokaribia, watu wa Gaza wako imara katika azimio lao la kudumisha ibada ya Jamaa. Katika eneo hilo linalokumbwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel, Swala ya Ijumaa ya jamaa imeshuhudia wimbi la waumini bila kukatishwa tamaa na uharibifu wa vita.

Akizungumza na Al Jazeera, Mpalestina  mmoja alisisitiza mwendelezo wa ibada katika eneo hilo, akisema, "Swala hazijawahi kukoma katika msikiti huu; ulikuwa ukilengwa na Waisraeli usiku na bila ya onyo."

Aliendelea kutangaza, "Tuna msimamo thabiti kuhusu kudumisha Adhana," akisisitiza juhudi za kusafisha eneo ndogo ndani ya uwanja mkubwa wa msikiti ili kuendelea na swala za jamaa kila siku.

Azimio la Waislamu wa eneo linaonekana wazi wakati wanaendana na mazingira magumu, huku afisa Mpalestina huyo akisisitiza kuwa, "Tutaendelea kuswali hata njiani na kwenye magofu."

Mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya Gaza yameua takriban watu 31,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Uvamizi huo wa kijeshi pia umesababisha 85% ya watu milioni 2.3 kukimbia makazi yao huko Gaza, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa. Aidha utawala haramu wa Israel umelenga kwa mabomu misikit, makanisa, shule, hospitali na nyumba za makazi ya raia katika uharibifu ambao bila shaka ni jinai za kivita.

Habari zinazohusiana
captcha