IQNA

Kadhia ya Palestina

Baraza la Usalama lapitisha azimio dhaifu kuhusu Gaza, lashindwa kusitisha jinai za Israel

6:46 - December 23, 2023
Habari ID: 3478078
IQNA-Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hatimaye limepitisha azimio kuhusu jinai za Israel dhidi ya Gaza, likidai kuongezwa kwa misaada katika eneo lililozingirwa lakini lakini limeshindwa kuulazimisha utawala haramu wa Israel usitishe vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika eneo hilo.

Azimio hilo dhaifu limepasishwa kufuatia mashinikizo ya kimataifa kwa Marekani -ambayo ni muungaji mkono mkuu wa utawala ghasibu wa Israel. Baraza la Usalama limetaka utawala katili wa Israel usitishe mashambulio yake ya kinyama dhidi ya Gaza unayoyafanya kwa lengo la kulipiza kisasi kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya wapigania ukombozi wa Palestina. Azimio hilo ambalo limepitishwa usiku wa kuamkia leo lilipitish linataka kuongezwa zaidi misaada wa kibinadamu kwa ajili ya Gaza.

Azimio lililopitishwa pia linamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumteua Mratibu Mwandamizi wa Masuala ya Kibinadamu na Ujenzi, ili awajibike kuwezesha, kuratibu, kufuatilia na kuthibitisha huko Gaza, "hali ya kibinadamu ya shehena zote za misaada ya kibinadamu zinazopelekwa Gaza zinazotumwa na Mataifa ambayo sio sehemu ya mzozo. Lengo ni kuharakisha utoaji wa misaada ya kibinadamu.

Azimio hilo linazitaka pande zinazohusika katika mzozo huo kushirikiana na mratibu, ambaye atapewa mamlaka ya kuripoti kwa Baraza la Usalama kuhusu kazi yake ndani ya siku 20 kwa mara ya kwanza, na kila siku 90 baada ya hapo.

Baada ya mazungumzo makali ya faragha kwa wiki nzima katika Baraza la Usalama lenye wanachama 15 (watano wa kudumu), mabalozi wamepiga kura asubuhi hii ya saa za New York Marekani kuhusu rasimu ya azimio lililoandikwa na Umoja wa Falme za Kiarabu ambalo limeripotiwa kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuruhusu utoaji wa misaada kwa usalama na bila vikwazo kwa raia walioathirika katika Ukanda wa Gaza.

Azimio hilo lililofadhiliwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, ilipitishwa kufuatia mazungumzo ya siku kadhaa juu ya maneno yake, ambapo ilipunguzwa  makali yake dhidi ya Israel kwa ombi la Marekani.

Baadhi ya nchi zinazokosoa hujuma ya Israel zimekuwa zikisisitiza kwamba azimio lolote la kulaani Hamas, lazima pia lilaani uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza na maelfu ya vifo vya raia vilivyotokana na hatua ya kijeshi ya Israel tangu tarehe 7 Oktoba. 

Kura katika baraza hilo yenye wajumbe 15 ilikuwa 13-0 huku Marekani na Russia  zikijizuia kupiga kura.

Kura hiyo ilifuatia kura ya turufu ya Marekani kwa marekebisho yaliyopendekezwa na Russia ambayo kuhusi kusitishw akikamilifu vita vya Israel dhidi ya Gaza.

Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa Vasily Nebenzya aliikashifu Marekani, akisema "wametumia mbinu wanayoipenda zaidi... ya mabavu", na amelitaja azimio hilo kuwa maandishi yasiyo na makali yoyote. Russia imekuwa ikisisitiza kuwa lazima Israel ishurutisweh kusitisha vita dhidi ya Wapalestina.

Israel imeshambulia Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, na kuua Wapalestina 20,057, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine 53,320, kulingana na mamlaka ya afya katika eneo hilo.

Mashambulizi ya Israel yameifanya Gaza kuwa magofu huku nusu ya makazi ya eneo la pwani yakiharibiwa, na karibu watu milioni 2 wamelazimika kuyahama makazi yao ndani ya eneo hilo lenye watu wengi kutokana na uhaba wa chakula na maji safi.

Hamas yakosoa azimio

Wakati huo huo Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa mjibizo kwa azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa halitoshi na halikidhi mahitaji.

Hamas imesisitiza kuwa kupitishwa kwa azimio hilo hakulingani na mahitaji na matakwa ya hali mbaya ya maafa yanayoshuhudiwa hivi sasa katika Ukanda wa Gaza.
 
Harakati hiyo imeongeza kuwa serikali ya Marekani imewasilisha azimio hili kwa namna ambayo inatoa ruhusa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuendeleza mauaji na uharibifu.

3486515

Habari zinazohusiana
captcha