IQNA

Jinai za Israel

Wataalamu kujadili ugaidi wa Israel na kufeli sheria za kimataifa

16:38 - November 28, 2023
Habari ID: 3477957
TEHRAN (IQNA) – Kundi la wataalam kutoka nchi mbalimbali watafanya mkutano wa kimataifa tarehe 29 Novemba 2023, kujadili kufeli sheria za kimataifa na mashirika ya kuwalinda Wapalestina katika kukabiliana na ugaidi wa kiserikali wa utawala haramu Israel.

Kongamano hilo ambalo litafanyika kwa njia ya intaneti limeandaliwa na  Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), chini ya anuani ya "Ugaidi wa Israel na Kushindwa kwa Sheria ya Kimataifa za Kibinadamu."

Hafla hiyo itashirikisha Seyyed Jafar Razavi, mtaalam wa masuala ya Asia Magharibi, Dk. Baqer Darwish, rais wa Jukwaa la Haki za Kibinadamu la Bahrain, Dk Amiruddin Jahaf, mkuu wa Kundi la Haki za Kibinadamu la Yemen, Dk Yasser Abu Heen, the mkuu wa Umoja wa Vyombo vya Habari vya Palestina, na Iyad Abu Nasser, mfungwa wa zamani wa Palestina kutoka Gaza, na Ali Al-Sahib, na mchambuzi wa Iraq.

Wazungumzaji watawasilisha maoni na uzoefu wao juu ya ukiukaji wa haki za binadamu wa Israel na sheria za kimataifa huko Palestina, haswa katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa.

Wataalamu pia watajadili nafasi na wajibu wa jumuiya ya kimataifa na mashirika ya kimataifakatika kulinda haki za watu wanaodhulumiwa.

Kikao hicho cha intaneti au Webinar kitaanza  saa nne asubuhi kwa majira ya UTC na kitarushwa moja kwa moja au mubasahra kupitia  ukurasa wa IQNA kwenye tovuti ya video ya Aparat.

Tukio hilo linakuja huku vita vya siku 49 vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza vikwa vimewaua Wapalestina wasiopungua 15,000 wakiwemo watoto 6,150 na zaidi ya wanawake 4,000.

Utawala huo vamizi pia uliharibu maelfu ya nyumba, shule, hospitali, misikiti, makanisa na miundombinu muhimu , na kuwaacha mamia ya maelfu ya watu bila makazi na watu wote zaidi ya milioni mbili Gaza bila umeme na maji.

3486209

Habari zinazohusiana
captcha