IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

Spika wa Bunge la Iran: Operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa imeibua mabadiliko katika mlingano wa kimataifa

20:42 - November 04, 2023
Habari ID: 3477838
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema: Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ilibadilisha m mpangilio mlingano wa mfumo wa kimataifa.

Mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, wanajeshi wa makundi  ya wapigania ukombozi au wanamuqawama wa Palestina walianzisha operesheni ya kushtukiza iitwayo "Kimbunga cha Al-Aqsa" kutoka Gaza (kusini mwa Palestina) dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni wa Israel ili kujibu jinai za mara kwa mara za utawala huo dhidi ya Wapalestina. Katika kulipiza kisasi pigo hilo la kihistoria, utawala ghasibu wa Israel ulishadidisha mzingiro katika Ukanda wa Gaza na tokea siku hiyo umekuwa ukidondosha mabomu dhidi ya raia wa Gaza.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina ametangaza kuwa, idadi ya mashahidi huko Gaza imefikia zaidi ya elfu 9,200 na idadi ya waliojeruhiwa imefikia zaidi ya elfu 23.

Kuhusiana na hili, Mohammad Baqir Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran katika hotuba kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa ameeleza kuwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ilibadilisha malingano wa mfumo wa  dunia na kuongeza kuwa: "Vyovyote vile wafanyavyo, wakuu wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel hawawezi kuirejesha dunia katika hali ya awali ya kabla ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa."

Akigusia uungaji mkono wa watetezi wa uhuru duniani kwa watu wa Gaza na Palestina, Spika Bunge la Iran amesema: "Mwisho wa njia ya mchakato kuanzisha uhusiano na Israe ni kushindwa na kufilisika na na mwisho wa njia ya muqawama na mapambano  ni ushindi, fahari na heshima.

Spika wa Bunge la Iran amesisitiza kuwa: "Makundi ya muqawama au mapambano hayaegemei kwa serikali, bali ni suala linalotokana na umma wa Kiislamu na linalotokana na imani ya kupambana dhidi ya ukatili, jinai na dhulma na hakuna shaka kuwa watenda jinai wa Israel wataonja uchungu wa kushindwa "

Leo Jumamosi tarehe 13 mwezi Aban kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani ya Hijria Shamsia ambayo ni sawa na tarehe Nne Novemba Miladia inatambulika hapa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari wa Kimataifa.

Itakuumbukwa kuwa, miaka 44 iliyopita katika siku kama ya leo tarehe 13 mwezi Aban mwaka 1358 Hijria Shamsia sawa na Novemba Nne mwaka 1979 wanachuo wa Iran waliliteka pango la ujasusi la ubalozi wa Marekani hapa Tehran kulalamikia njama mbalimbali zilizokuwa zikitekelezwa na serikali ya Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Mamilioni ya wananchi, hasa wanafunzi kote Iran wamejitokeza katiak maandamano yaliyofanyika katika miji mbali mbali nchini kwa mnasaba wa siku hii adhimu.

4179733

Habari zinazohusiana
captcha