IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Misikiti ya London yapokea barua za chuki dhidi ya Uislamu baada ya mitetemeko ya ardhi Uturuki-Syria

20:30 - February 17, 2023
Habari ID: 3476576
TEHRAN (IQNA) – Takriban misikiti miwili mjini London imepokea barua za chuki dhidi ya Uislamu kufuatia mitetemeko mikubwa ya ardhi nchini Uturuki na Syria ambayo imesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu.

Barua ya kutatanisha ilitumwa kwa msikiti wa Masjid Ramadan huko Hackney, London mashariki, Jumatano na Polisi wa Metropolitan walithibitisha msikiti mwingine wa London mashariki pia ulilengwa.

Mwenyekiti wa msikiti wa Masjid Ramadan Erkin Guney ameshtushwa na barua hiyo.

Barua kwa msikiti wa kwanza wa Kituruki nchini Uingereza ilisomeka hivi: "Sikuweza kuacha kutabasamu nikitazama watu wakitolewa kwenye vifusi, wengine wakiwa wamekufa, wengine, inasikitisha, wamenusurika na kubakia hai."

Barua hiyo pia ilisema "kadiri Waislamu wanavyoteseka ndivyo bora zaidi" na mwandishi alisema wanatamani tetemeko lingine la ardhi lijiri katika eneo hilo.

Bw Guney alisema: "Nimeumizwa sana na barua hii  kuona mtu anatuma barua hii wakati wa hali mbaya kama hiyo.”

“Namuombea mwanaume huyo apate mapenzi. Ninasikitika kuwa ... mnamo 2023 tunapaswa kuwa na chuki nyingi dhidi ya wanadamu.

Polisi imesema imepokea ripoti ya barua iliyotumwa kwa misikiti miwili ya Hackney yenye lugha ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu.

Ikumbukwe kuwa Februari sita mitetemeko miwili mikubwa ya ardhi yenye ukubwa wa 7.8 na 7.5 kwa kipimo cha Rishta iliyakumba maeneo ya kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria. Hadi sasa karibu watu elfu 45 wameripotiwa kuaga dunia katika janga hilo la kimaumbile.  Aidha malaki ya watu wamejeruhiwa huku idadi kubwa ya nyumba zikiharibia na hivyo kupelekea mamilioni ya watu kuhitajia misaada ya dharura.

3482508

captcha