IQNA

Nakala 15,000 za Qur'ani Tukufu zasambawza miongoni mwa waathirika wa Zilzala Uturuki

21:00 - February 20, 2023
Habari ID: 3476592
TEHRAN (IQNA) – Takriban nakala 15,000 za Kurani Tukufu zimetumwa katika maeneo yaliyokumbwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi nchini Uturuki ya tarehe 6 Februari.

Mtendaji mkuu wa Wakfu wa Diyanet wa Uturuki (TDV), amesema kuwa taasisi hiyo imetuma nakala hizo na idadi itaongezeka katika siku zijazo.

"Kulikuwa na mahitaji makubwa ya Qur'ani Tukufu katika maeneo yaliyokumbwa na mitetemeko ya ardhi.Tulituma Qur’ani 15,000 na nakala mpya sasa zinachapishwa, "naibu mkuu ya Bodi ya Wadhamini İhsan Açık alisema.

Açık alisema kuwa mbali Misahafu, vitabu vya watoto vinavyozingatia dini pia vitatumwa kwa waathirika wa mitetemeko ya ardhi. "Sehemu ya vitabu vya watoto wetu vimefikia mkoa. Tuko katika juhudi kwamba kila mtoto (katika eneo la zilzala) ana kitabu cha watoto mkononi," alisema.

Açık pia alisema kuwa wamekuwa wakiwatuma maafisa wa kidini katika mkoa huo kufanya huduma ya "uongozi wa kiroho." “Waelekezi wetu wa kiroho wameanza kwenda katika eneo hilo. Wananchi wetu wana maswali mengi ya kiroho. Wengi wanahitaji watu wa kusikiliza shida zao. Diyanet yetu imekuwa ikijaribu kuwasaidia waathiriwa wa mitetemeko la ardhi tangu siku ya kwanza ya matetemeko hayo,” alisema.

Ikumbukwe kuwa Februari sita mitetemeko miwili mikubwa ya ardhi yenye ukubwa wa 7.8 na 7.5 kwa kipimo cha Rishta iliyakumba maeneo ya kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria. Hadi sasa karibu watu elfu 46 wameripotiwa kuaga dunia katika janga hilo la kimaumbile wengi wakiwa nchini Uturuki.

3482540

 

 

captcha