IQNA

Zilzala Uturuki na Syria

Katibu Mkuu wa OIC atembelea Uturuki kufuatia matetemeko ya ardhi

21:14 - February 22, 2023
Habari ID: 3476606
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amefanya ziara rasmi nchini Uturuki kufuatia matetemeko makubwa ya ardhi yaliyoikumba nchi hiyo zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Katika siku ya kwanza ya safari yake siku ya Jumatano, Hissein Brahim Taha alisafiri hadi Gaziantep na kufanya mikutano na gavana Davul Gül na meya Fatma Şahin.

Taha amebainisha kuwa anazuru Uturuki kwa niaba ya nchi zote wanachama wa OIC, akitoa wito kwa mataifa yote ya Kiislamu kuunga mkono Uturuki kufuatia maafa hayo ya kimaumbile.

Taha pia ameratibiwa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Cavusoglu mjini Ankara siku ya Alhamisi.

Ziara hiyo inafanywa ili kuonyesha mshikamano wa OIC na watu wa Uturuki na kuongeza muda wa rambirambi kutokana na matetemeko mawili ya ardhi ambayo yamepelekea zaidi ya watu 42,300, kupoteza maisha hadi sasa.

Mitetemeko hiyo ya ukubwa wa 7.7 na 7.6 ilijikita Kahramanmaras na kugonga majimbo mengine 10 ya kusini - Hatay, Gaziantep, Adiyaman, Malatya, Adana, Diyarbakir, Kilis, Osmaniye, Sanliurfa na Elazig. Zaidi ya watu milioni 13 wameathirika. Aidha maeneo ya kusini mwa Uturuki pia yalikumbwa na matetemeko hayo na kupelekea watu wasiopungua 5000 kupoteza maisha hadi sasa.

3482572

Kishikizo: zilzala uturuki syria oic
captcha