IQNA

Wamagharibi na ugaidi

Majasusi wa Kanada na Uingereza walisafirisha wasichana kujiunga na magaidi wa Daesh

17:15 - August 31, 2022
Habari ID: 3475710
TEHRAN (IQNA)- Mwandishi wa kitabu kilichochapishwa hivi karibuni amefichua jukumu la idara ya kijasusi ya Kanada (Canada) katika kutuma wasichana kwenda kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na kusisitiza kuwa serikali ya Uingereza ilijua jukumu la Kanada katika kashfaa hii lakini ikajizuia kuifichua.

Kisa cha Shamima Begum, raia wa zamani wa Uingereza ambaye alijiunga na ISIS mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 15, bado kina utata.

Mwaka jana, serikali ya Uingereza ilifuta uraia wake wa Uingereza alipokwenda Syria kujiunga na ISIS; Lakini sasa imebainika kuwa kuwa aliingizwa nchini Syria kinyemela na mtu aliyekuwa akifanya kazi katika idara ya ujasusi ya Kanada, na kwamba Uingereza ilifunika kwa makusudi jukumu la Canada.

The Secret History of the Five Eyes : The Untold Story of the Shadowy International Spy Network ni kitabu kilichoandikwa na Richard Kerbage, ripota wa usalama wa zamani wa Sunday Times, na wa kijasusi unaojumuisha mashirika ya kijasusi ya Australia, Kanada, New Zealand, Uingereza, na Marekani.

Kanada pia ilifahamu kuwa jasusi aliyehusika katika kusafirisha wasichana wajiunga na ISIS alikuwa pia jasusi wa pande mbili ambaye alikuwa akihudumu kama jasisi ya ISIS na pia jasusi wa Shirika la Ujasusi la Kanada (CSIS).

Baada tu ya kukamatwa kwa jasusi aliyetajwa nchini Uturuki, Canada iliifahamisha Uingereza kwa siri kuhusu kadhia hii na ikataka  habari za kuhusika Kanada zisifichuliwe.

Msemaji wa Huduma ya Ujasusi ya Usalama wa Kanada alisema hawezi kuthibitisha hadharani au kukataa maelezo ya uchunguzi huo.

Msemaji wa serikali ya Uingereza pia alidai: Ni sera yetu ya muda mrefu kutotoa maoni juu ya masuala ya taarifa kijasusi.

Shamima Begum, mwenye umri wa miaka 23 ambaye anazuiliwa katika kambi moja kaskazini mashariki mwa Syria kutokana na kunyimwa uraia wake wa Uingereza, alisema: "Inaonekana kwamba ukusanyaji wa taarifa za kijasusi ni kipaumbele cha serikali ya Uingereza na wala serikali hii haijali kuhusu watoto."

Shamima Begum aliyezaliwa na wazazi wa Bangladesh, aliondoka London mwaka wa 2015 alipokuwa na umri wa miaka 15 na kusafiri hadi Syria kupitia Uturuki pamoja na wasichana wengine wawili wa shule. Huko Syria, aliolewa na gaidi wa ISIS.

Begum alipatikana katika kambi mnamo 2019. Serikali ya Uingereza ilibatilisha uraia wake na kutangaza kuwa alikuwa tishio la usalama.

408216

captcha