iqna

IQNA

mitetemeko
Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) – Takriban misikiti miwili mjini London imepokea barua za chuki dhidi ya Uislamu kufuatia mitetemeko mikubwa ya ardhi nchini Uturuki na Syria ambayo imesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu.
Habari ID: 3476576    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/17

Zilzala Uturuki na Syria
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) ametoa wito kwa Waislamu walionuia kutekeleza safari ya ibada ya Hija ndogo ya Umrah kusitisha safari hiyo kwa sasa na badala yake kutumia fedha hizo kuwasaidia wahanga wa mitetemeko (zilzala) ya ardhi Uturuki na Syria.
Habari ID: 3476559    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/14

Zilzala Syria na Uturuki
TEHRAN (IQNA)-Matumaini ya kupata manusura zaidi chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa mitetemeko miwili mikubwa ya ardhi Jumatatu iliyopita katika nchi za Syria na Uturuki yanazidi kupungua siku 5 baada ya maafa hayo ambapo idadi ya walipoteza maisha hadi sasa ikifika 25,000 huku Umoja wa Mataifa ukitabiri kuwa yamkini idadi hiyo ikaongezeka maradufu.
Habari ID: 3476547    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/11

Mitetemeko Uturuki na Syria
TEHRAN (IQNA) – Watu katika nchi za Balkan Magharibi za Kosovo na Macedonia Kaskazini wamejipanga kusaidia Uturuki baada ya mitetemeko ya ardhi yenye ukubwa wa 7.7 na 7.6. kupelekea karibu watu elfu 20 kupoteza maisha hadi sasa huku idadi kubwa yanyumba zikiwa zimeharibiwa Uturuki na Syria.
Habari ID: 3476539    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/09

Misaada kwa Syria
TEHRAN (IQNA)- Shehena ya tano ya misaada ya kibinadamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa watu waliokumbwa na mitetemeko ya ardhi nchini Syria iliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus mapema leo Alhamisi.
Habari ID: 3476537    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/09

Rais Assad wa Syria
TEHRAN (IQNA)- Rais Bashar al-Assad wa Syria amefichua kuwa Marekani inatoa mashinikizo kwa nchi zinazotaka kuwasaidia waathirika wa mitetemeko ya ardhi nchini Syria. Assad ameyasema hayo katika mkutano na ujumbe wa mawaziri kadhaa wa Lebanon.
Habari ID: 3476535    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/09