IQNA

Fitina baina ya Waislamu

Kusitishwa uonyeshaji Filamu ya 'Mwanamke wa Mbinguni' nchini Uingereza

21:30 - June 08, 2022
Habari ID: 3475351
TEHRAN (IQNA)- Kampuni iliyotengeneza filamu yenye utata na yenye kuibua mifarakano ya 'Lady of Heave'n au 'Mwanamke wa Mbinguni' imetangaza kuwa imesitisha uonyeshaji wa flamu hiyon chini Uingereza kufuatia maandamano na malalamiko ya watu wengi nchini humo

Kwa mujibu wa taarifa, Shirika la Cineworld   ambalo limetayarisha filamu hiyo yenye utata limeghairi kuonyeshwa kwake nchini Uingereza siku ya Jumanne, kufuatia maandamano ya Waislamu mbele ya kumbi za sinema kupinga filamu hiyo.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii pia walitayarisha ombi la mtandaoni lililotiwa saini na zaidi ya watu zaidi ya 120,000 kupinga kuonyeshwa filamu  ya 'Lady of Paradise', waliyoiita ya kufedhehesha, yenye kuvunjia heshima matukufu wa kidini na pia yenye kuibua malumbano ya kimadhehebu.

Wengi katika miji ya Uingereza walifanya maandamano wakielezea filamu hiyo kama tusi kwa Uislamu.

Filamu hii ya Uingereza iliyoongozwa na "Eli King", ambayo ilianza kuonyeshwa katika kumbi za sinema za Uingereza Ijumaa iliyopita, ni filamu ya kwanza ambayo, kwa tafsiri yake, inadai kuonyesha maisha ya Bibi Fatima Zahra (SA) na Imam Ali ibn Abi Talib (AS).

Tume ya Kiislamu ya  Haki za Kibinadamu mjini London ilisema katika taarifa yake kuwa: "Filamu hii, kwa taswira yake ya kufedhehesha ya watu mashuhuri wa Kiislamu katika siku za mwanzo za Uislamu, wakiwemo wake za Mtume Muhammad (SAW), ni uchochezi wa wazi na ni jaribio la aibu la kuleta mifarakano na mikwaruzano katika Umma wa Kiislamu."

Aidha wanazuoni wa Kiislamu wa madhehebu wa Shia wamekosoa vikali filamu hiyo kwa utafiti wake duni na pia kutokana na malengo yake ya kichochezi.

Miaka kadhaa nyuma wakati taarifa za kutayarishwa filamu hiyo zizlipoenea na ilipobainika malengo yake, wanazuoni wa ngazi za juu wa Kishia nchini Iran waliipinga vikali na wakatoa wito kwa Waislamu kutoitazama miongoni mwa walioipinga ni  Ayatullah Lotfollah Safi Golpayegani, Ayatullah Nasser Makarem Shirazi, na Ayatullah Hossein Ali Nouri Hamaedani.

4062722

captcha