IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Makombora ya Jihad Islami yaliwafanya Wazayuni wakimbilie mapangoni na kuomba usitishaji vita

20:09 - August 12, 2022
Habari ID: 3475611
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema maroketi na makombora kutoka Ukanda wa Gaza yaliwafanya walowezi wa Kizayuni wakimbilie mapangoni mwao kutafuta hifadhi na kulazimika kufanya mapataano na kusitisha mapigano.

Katika hotuba za Sala hiyo, Hujjaatul Islam Kazem Seddiqi amezungumzia mashambulio ya karibuni ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na jinai ulizofanya dhidi ya wananchi wa Palestina na akasema: wakati Israel iliweza kushinda Vita vya Siku Sita na Waarabu, kwa kuzaliwa Hizbullah ya Lebanon, ngano za kutoshindika utawala wa Kizayuni zilibatilishwa kwa nguvu na uwezo mkubwa wa Muqawama katika Vita vya Siku 33.

Hujjatul Islam Seddiqi amebainisha kuwa, katika vita vya karibuni pia, japokuwa si vikosi vyote vya muqawama vilivyoshiriki, Jihadul Islami ilifyatua mamia ya maroketi na makombora kutoka Ukanda wa Gaza yaliyowafanya walowezi wa Kizayuni wakimbilie mapangoni mwao kutafuta hifadhi na kulazimika kufanya mapataano na kusitisha mapigano.

Kuhusiana na kurushwa satalaiti ya Iran ya Khayyam kuelekea anga za mbali, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema: kutumwa satalaiti hiyo angani ni miongoni mwa mafanikio mapya ya kielimu ya Iran ambayo yamepatikana kwa umakini, umoja, kutawakali, kuwa na matumaini, kushikamana na uongozi wa kidini na kuwa na imani na njia inayowezesha kufikia malengo ya nchi.

Kwingineko, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran pia amesisitiza kuchukuliwa hatua zipasazo katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran.

Hujjaatul Islam Kazem Seddiqi ameashiria mwenendo wa mazungumzo ya uondoaji vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran na akasema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ingali inatekeleza ahadi na wajibu wake. Ni wahusika wa upande wa pili ndio waliohalifu ahadi na makubaliano na kuamua kutoheshimu makubaliano ya kimataifa ya JCPOA.

4077545

Habari zinazohusiana
captcha