IQNA

Jina za Israel

Umoja wa Mataifa washtushwa na kugunduliwa kwa kaburi la umati Gaza

11:30 - April 23, 2024
Habari ID: 3478724
IQNA - Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameitaja ripoti kuhusu kugunduliwa kwa makaburi ya halaiki huko Gaza kuwa ni ya kushtusha, huku ushahidi wa awali ukionyesha utawala haramu wa Israel umehusika katika jinai hiyo.

Stephane Dujarric alitoa wito wa uchunguzi  huru na "wa kuaminika" katika maeneo ambayo makaburi yanapatikana. Ametoa tamko hilo  katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu alipoulizwa kuhusu kufichuliwa kwa angalau miili 283  katika kaburi la umati katika Hospitali ya Nasser katika mji wa kusini wa Khan Yunis.

Wakati huo huo Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita wa Israel katika Hospitali ya Nasser huko Gaza ambapo mamia ya miili ya raia imeopolewa kutoka kwenye makaburi ya umati.

 

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu jumuiya hiyo yenye wanachama 57 ililaani mauaji na kuzikwa kwa umati mamia ya wananchi wa Gaza katika uwanja wa Hospitali ya Nasser kuwa ni "uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na ugaidi wa serikali."

OIC imebainisha waliouawa ni timu za matibabu, wagonjwa na wakimbizi waliokuwa  katika Hospitali ya Nasser.

Shirika hilo lilisema zaidi kwamba "mamia ya waliokimbia makazi yao, waliojeruhiwa, wagonjwa na timu za matibabu wameteswa na kunyanyaswa kabla ya kunyongwa na kuzikwa kwa umati".

 OIC imezitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu na Mahakama ya Kimataifa ya Haki katekeleza majukumu yao kuhusu jinai hii.

Wafanyakazi wa utumishi wa umma huko Gaza wameopoa miili ya Wapalestina 283 katika makaburi kadhaa ya umati katika yadi ya Hospitali ya Nasser, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee. Baadhi ya waliouawa walikuwa wamefungwa macho na kufungwa pingu.

Shirika la Afya Ulimwenguni lilisema mnamo Aprili 6 kwamba hospitali kubwa zaidi ya eneo la Palestina, al-Shifa, imeharibiwa kabisa mwezi mwezi uliopita katika hujuma ya Israel.

Takriban Wapalestina 34,097 wameuawa; wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na watu wengine 76,980 wamepata majeraha. Zaidi ya Wapalestina milioni 1.7 wamekuwa wakimbizi wa ndani huko Gaza tangu Oktoba 7 wakati Israel ilipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo.

3488046

Habari zinazohusiana
captcha