IQNA

Kadhia ya Palestina

Raisi: Kuunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa ni kigezo cha heshima kwa mataifa

13:30 - November 10, 2023
Habari ID: 3477868
TEHRAN (IQNA) - Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, nchi zinazoinukia kiuchumi na nchi zinazoendelea zina uwezo mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika kuchangia msingi wa mfumo mpya wa dunia.

Rais Ebrahim Raisi amesema hayo Alhamisi huko Tashkent Uzbekistan katika Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi (ECO), na kubainisha kuwa, hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono na ikishirikiana na mataifa mengi huru na washirika wake wa kimataifa, inafuatilia suala la kuanzisha mfumo wa haki na kiadilifu ambao umejengeka juu yay msingi wa kuheshimiana na kuimarisha ushirikiano wa pande kadhaa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iranpress, Seyed Ebrahim Raisi ametangaza uungaji mkono usio na masharti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ECO na shughuli zake katika mkutano wa 16 wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya ECO huko Tashkent, mji mkuu wa Uzbekistan, na kusisitiza kwamba tumeazimia kutoa msaada, rasilimali zaidi na nishati kwa minajili ya kuboresha zaidi ushirikiano.

Aidha katika hotuba yake hiyo kwenye mkutano huo, Rais wa Iran amekosoa na kulaani jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza.

Vilevile, mwishoni mwa sehemu ya kwanza ya hotuba yake iliyohusiana na jinai za utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono wananchi madhulumu na wenye kusimama kidete wa Gaza, Raisi alisimamisha hotuba hiyo kwa dakika chache na kuwataka hadhirina  kuwasomea Surat al-Fatiha mashahidi wa Gaza.

Rais wa Iran kadalika ameeleza kwamba, hii leo, kuunga mkono Palestina na watu wanaodhulumiwa wa Gaza ni kigezo cha heshima kwa mataifa.

Kadhalika amesema, jinai za kutisha za utawala wa Kizayuni katika mashambulizi dhidi ya hospitali, shule, vyuo vikuu na kambi ya wakimbizi ya Jabalia, na kusababisha kuuawa shahidi na kujeruhi mamia ya wakimbizi, wagonjwa, majeruhi wananchi wa Palestina wasio na ulinzi na wasio na makazi, ni mambo yanayoonyesha utambulizi wa kivamizi wa utawala huo na mfano wa wazi wa mauaji ya kimbari na jinai  dhidi ya ubinadamu.

4180862

Habari zinazohusiana
captcha