IQNA – Tarehe 15 Oktoba, katika Msikiti Mkuu wa Astana, Kazakhstan, mashindano ya pili ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur'an Tukufu yamekamilika, yakileta pamoja washiriki 22 kutoka mataifa 21. Tukio hili limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Kiislamu ya Saudi Arabia na Mamlaka ya Kiroho ya Waislamu wa Kazakhstan.
IQNA – Dar al-Ifta ya Misri imetoa fatwa mpya ya kidini inayoruhusu raia kuelekeza mali ya zakat kusaidia mahitaji ya msingi ya watu waliokoseshwa makazi huko Gaza.
IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya 26 ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind bint Maktoum imeanza rasmi Dubai, ikiwakutanisha wanaume na wanawake wanaohifadhi Qur’ani kutoka kote katika Muungano wa Falme za Kiarabu.
IQNA – Kijana mmoja wa Kipalestina amegundua nakala ya Msahafu ikiwa salama kabisa chini ya magofu ya nyumba yake iliyoharibiwa kaskazini mwa Gaza, akieleza hisia za kina na shukrani baada ya miezi ya mashambulizi.
IQNA – Imamu Mkuu wa Al-Azhar nchini Misri, Sheikh Ahmed al-Tayeb, amesisitiza umuhimu wa kuheshimu matukufu ydini na kuepa uka matusi au dharau dhidi matukufu yao.
IQNA-Idara Kuu ya Mambo ya Kiislamu, Awqaf na Zakat ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imetangaza kuanza kwa usajili wa toleo la pili la Emirates International Quran Award.
IQNA – Baada ya miezi kadhaa ya kufungwa kutokana na mashambulizi ya angani, Msikiti wa Al-Tawhid ulioko katika kambi ya wakimbizi ya Al-Shati, Gaza, umefunguliwa tena na sauti ya adhana imeanza kusikika kwa mara nyingine.
IQNA – Neno Ta’avun (ushirikiano) hutumika kama istilahi ya kielimu katika fani nyingi, lakini katika Seerah ya Mtume Mtukufu (SAW), mara nyingi linahusiana na vitendo vinavyolenga kutimiza mahitaji ya wengine.
IQNA – Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yatafanyika wakati wa toleo la pili la Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Libya, yatakayofanyika mjini Tripoli mwishoni mwa mwezi huu.
IQNA – Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran, yakihusisha washiriki 330 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, yatafanyika mwaka huu katika mji wa Sanandaj ulioko magharibi mwa Iran, chini ya kauli mbiu: “Qur'ani, Kitabu cha Umoja.”
IQNA – Uislamu umeamuru wafuasi wake kusaidiana katika kutenda mema. Wakati watu wanapokusanyika na kuanzisha mahusiano ya kijamii, roho ya umoja huingia katika mahusiano yao, na hivyo hujikinga dhidi ya mgawanyiko na kutengana.