IQNA

Mtazamo wa Maadili Katika Qur'ani/ 4

Qur’ani Tukufu inakataza tabia ya udaku

20:00 - March 09, 2024
Habari ID: 3478476
IQNA - Udaku ni aina ya kusengenya ambapo mwenye kufanya hivyo humuambia mtu kile ambacho mtu mwingine amesema bila ridhaa yake.

Tabia hii inahusisha kufichua siri na kusababisha maovu na ndio maana Uislamu umeharamisha.

Hakuna shaka kuwa, tabia hii isiyofaa inadhoofisha mahusiano ya kibinadamu na kijamii na kukata urafiki, ukarimu na kuvuruga imani.

Qur’ani Tukufu inasema katika Aya ya 1 ya Surah Al-Humazah: "Ole wake kila mchongezi (safihi au mzushi) na msengenyaji.

Vile vile tunasoma katika Aya ya 11 ya Surah Al-Qalam: “(Mwenyezi Mungu anajua sana) Mwenye kukashifu, akizungukazunguka na kusengenyana.”

Aya hii inazungumza juu ya mtu ambaye huenda kwa watu kwa ajili ya kuwapigia kelele na kujenga uadui na chuki miongoni mwao. Mtu wa namna hiyo hueleza yale ambayo wengine wamesema kwa lengo la kuchochea tofauti na migogoro. Anadhoofisha urafiki na wema baina ya watu na anachochea fitna.

Kitendo hiki kimetajwa kuwa ni dhambi kubwa na hatari kwa sababu kinadhoofisha umoja wa watu katika jamii.

Qur’ani Tukufu inasisitiza kwamba watu hawapaswi kumwamini mzushi na mtu kama huyo anapaswa kutengwa katika jamii.

Mfano wa hadithi katika miaka ya mwanzo baada ya ujio wa Uislamu ulikuwa ule wa wanafiki ambao, baada ya kushindwa kuukabili Uislamu na Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) moja kwa moja, walijaribu kudhoofisha dini kwa unafiki na hadithi.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 6 ya Surah Al-Hujurat: “ Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.”

3487410

captcha