IQNA

Fikra za Kiislamu

Mtazamo wa Imam Ali (AS) kuhusu kusengenya

7:00 - November 01, 2022
Habari ID: 3476016
TEHRAN (IQNA) – Katika khutba ya 140 ya Nahjul Balagha, Imam Ali (AS) anasisitiza kwamba kusengenya sio sahihi katika mfumo wowote maadili na anapendekeza watu wawatendee wenye dhambi kwa huruma.

Khutba za 140 na 141 zinahusu masuala ya kimaadili. Mtazamo wa Imam Ali (AS) wakati akikabiliana na suala hili ni tofauti na muhimu.

Katika Khutba  ya 140, anashauri watu wasijihusishe na usengenyaji na kutafuta makosa ya wengine. Kilicho muhimu hapa ni namna anavyoijadili mada.

Badala ya kueleza adhabu ya madhambi hayo huko Akhera, Imam Ali (AS) antumia mbinu ya hali ya mazungumzo na kusisitiza mambo mawili.

Kwanza, anaonyesha maswala ya kimantiki ya mtu anayejaribu kutafuta makosa kwa wengine. Hapa, Imam Ali (AS) anajaribu kuwaaminisha wengine kwamba kusengenya si kuzuri.

Pili, anaanzisha mazungumzo juu ya sifa mbaya ya kusengenya kama bila hata kutilia mkazo mtazamo wa kidini.  Anabainisha kuwa kwa mujibu wa kanuni za maadili, kusengenyana hakufai hata kwa wasio Waislamu na wasiofuata dini yoyote.

Kwa mujibu wa khutba hii, baadhi ya masuala ni muhimu katika mtazamo wa dini, lakini pia kuna baadhi ya masuala ambayo ni sehemu ya kanuni za maadili. Masuala haya ni pamoja na uaminifu, kutenda haki, kuwa mkweli, nk.

Kadhalika, kusengenya hakukubaliki chini itikadi yoyote ile ya kimaadili; kwa hivyo huna haja ya kuwa Muislamu kujiepusha na hili, badala yake, ukweli kwamba wewe ni binadamu unatosha kuepuka hili.

Jambo lingine katika khutba hii ni jinsi tunavyopaswa kuwatendea wale wanaojihusisha na usengenyaji.

Khutba inaanza na sentensi hii: "Wale ambao hawatendi dhambi na wamejaliwa kuwa mbali na dhambi wanapaswa kuwahurumia wakosefu na watu wengine wasiotii."

Ukweli kwamba Imam Ali (AS) anasema watu wanapaswa kuamiliana na wenye dhambi kwa huruma inavutia kwa sababu hisia za rehema na huruma hujitokeza wakati mtu fulani amekabiliwa na tatizo na sisi tunafikiria kumsaidia.

Hapa, anabainisha kwamba kuwahurumia watenda dhambi ni muhimu na hivyo ndivyo watu wanavyopaswa kuwaona wale wanaofanya dhambi.

Kwa hiyo, tukiwa na mtazamo huu, hatutajihusisha na usengenyaji na tutajaribu daima kuwarekebisha wakosefu.

Pia kuna nukta nyengine nyeti katika khutba hii kwani Imam Ali (AS) anawahutubia wale wanaofanya dhambi ya kusengenya.

Imam Ali (AS) anasema ikiwa umefanya madhambi na ukashuhudia dhambi ya mtu mwingine, huna budi kuitibu hali hii kwa njia tatu: sharti la kwanza ni kuwa nimetenda dhambi kubwa zaidi. Kwa hiyo, kwa vile Mwenyezi Mungu ameificha dhambi yangu, ninapaswa kutenda ipasavyo na nisiongelee dhambi za wengine.

Sharti la pili ni kwamba mtu afikirie kuwa nimefanya dhambi hii lakini hakuna mtu aliyegundua, hivyo si sawa kuwaambia wengine kuhusu dhambi ya ndugu yangu ambayo pia mimi nimewahi kuifanya

Sharti la tatu ni kwamba dhambi ninayoifanya si ndogo kuliko ile iliyofanywa na wengine kwa sababu kusengenya kunamaanisha kuwa ninafanya dhambi kubwa zaidi.

Na jambo la mwisho ni kwamba njia ya toba iko wazi daima na Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweza kuwasamehe waliofanya dhambi.

captcha