IQNA

Arbaeen 1445

Watoto washiriki katika vikao vya kusoma Qur'ani Tukufu katika Arbaeen

15:58 - September 05, 2023
Habari ID: 3477550
KARBALA (IQNA) – Watoto kadhaa wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali wanaonyesha ujuzi wao wa kusoma Qur'ani Tukufu wakiwa wanashiriki katika maandamano ya mwaka huu ya Arbaeen.

 Arbaeen ni neno la Kiarabu ambalo maana yake ni 40.  Katika muktadha huu, ni siku ya 40 tangu maadhimisho ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) na masahaba wake watiifu tarehe 10 Muharram katika siku ya Ashura. Mtukufu huyo aliuawa shahidi katika mapambano ya Karbala  karne 14 zilizopita.

Siku ya Imam Hussein (AS) ya Arbaeen inakuja tarehe 20 Safar, mwezi wa pili wa kalenda ya mwandamo wa Kiislamu.

Baada ya kufa shahidi Imam Hussein (AS) mikononi mwa katili Yazid bin Muawiya, watu ambao walishangazwa na ukatili wa ukoo wa Ummaya walianza kuzuru kaburi lake kutoa heshima zao na tokea wakati huo hadi leo vizazi katika umma wa Kiislamu vimeendeleza utaratibu huo. Kila mwaka idadi ya wafanyaziara katika Siku ya Arabeen inaongezeka ambapo mwaka uliopita idadi hiyo ilivunja rekodi na kufika milioni 21.

Arbaeen ya mwaka huu inakuja huku kukiwa na wimbi jipya la vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu vikiwa vinaripotiwa kwa wingi katika nchi za Ulaya, hasa Uswidi na Denmark, chini ya kivuli cha uhuru wa kujieleza.

Ifuatayo ni ripoti ya IQNA kutoka Iraq juu ya usomaji wa Qur'ani Tukufu miongoni mwa watoto.

Kishikizo: arbaeen
captcha