Sheikh Ibarahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria aliwaambia waandishi habari katika hafla hizo kwamba, mahudhurio yalikuwa makubwa mno na kwamba Imam Hussein alitaka kuleta mabadiliko katika Umma wa Kiislamu wakati huo ambapo Usilamu ulipaswa kutakaswa. Maombelezo ya Arbaini ya Imam Hussein (A.S) mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW yalifanyika pia katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan na India.
Nchini Iraq mamilioni ya wafanya ziara kutoka ndani na nje ya Iraq walikusanyika katika mji mtukufu wa Karbala na kushiriki katika mambolezo hayo muhimu.../mh