IQNA

Wanajihadi

Hizbullah yaonya itajibu vikali mashambulizi ya utawala dhalimu wa Israel

18:56 - January 27, 2024
Habari ID: 3478261
IQNA - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utapanua mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, utapata jibu kali na la sawasaw kutoka kwa harakati hiyo.

Sheikh Naim Qassem aliyasema hayo katika hafla iliyofanyika mjini Beirut na kusema iwapo vita vya Gaza hazijamalizika, basi vita dhidi ya Lebanon haviwezi kumalizika.

Iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaamau kuilenga Lebanon, "Hizbullah itaimarisha  vikosi vyake na kutoa jibu kali kwa adui, amebaini.

Sheikh Qassem aliendelea kutupilia mbali ukosoaji unaolenga Hizbullah kuwa eti haijatekeleza wajibu wake, akisema ukosoaji kama huo unapaswa kuelekezwa kwa nchi ambazo zimeshindwa kuwaunga mkono Wapalestina wanaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari kwenye Ukanda wa Gaza.

Amesema Hizbullah pia inatekeleza wajibu wake nchini Lebanon na vikosi vyake vimewaunga mkono watu wa Lebanon kwa juhudi za kila namna.

Rekodi za Hizbullah zinaonyesha kuwa chochote ambacho harakati hiyo imefanya kimekuwa kwa maslahi ya Lebanon, alisisitiza.

Tangu Oktoba 8, 2023, siku moja baada ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza kuanza, mpaka kati ya Lebanon na maeneo yanayokaliwa na Israel kumeshuhudiwa ufyatulianaji risasi, hasa kati ya jeshi la ghasibu la Israel na harakati ya Hizbullah.

Jana ripoti zilibaini kuwa wapiganaji wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon walishambulia kwa makombora vituo na ngome za kijeshi za Israel kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kusambaratisha mfumo wa kamera za usalama wa utawala huo haramu.

Kwa mujibu wa al-Mayadeen, Hizbullah imeharibu kikamilifu mfumo wa kamera za usalama wa utawala huo haramu uliosimikwa majuzi, kwa kuupiga kwa kombora la ardhini hadi ardhini la Falaq-1 katika mji wa Zar'it karibu na mpaka wa Lebanon.

Aidha wanajihadi hao wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah usiku wa kuamkia jana walishambulia kwa makombora kambi za kijeshi za utawala wa Kizayuni za Hunin Castle mjini Margaliot, Hanita, Avivim, Doviv , Metula na Shlomi karibu na mpaka wa Lebanon.

Hizbullah tayari imepigana vita viwili vya Israel dhidi ya Lebanon mwaka 2000 na 2006, na kulazimisha majeshi ya utawala huo kurudi nyuma katika mapigano yote mawili.

4196116

captcha