IQNA

Zifahamu Dhambi/ 4

Misamiati ya Qur'ani Tukufu inayohusu dhambi

21:11 - December 05, 2023
Habari ID: 3477991
TEHRAN (IQNA) – Katika lugha ya Qur'ani Tukufu na Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), kuna maneno mbalimbali yanayotumika kutaja madhambi.

21:11 - 2023/12/05

Kila moja ya maneno haya yanaangazia sehemu ya matokeo ya kutisha ya dhambi.

Maneno yaliyotumika katika Qur'ani Tukufu kutaja dhambi ni haya: 1- Dhanb, 2- Ma'siyah, 3- Ithm, 4- Sayyi'ah, 5, Jurm, 6-Haram, 7- Khati'ah, 8- Fisq. , 9-Fisad, 10-Fujur, 11-Munkar, 12- Fahisha, 13- Khibth, 14-Shar, 15-Lamam, 16- Wizr na Thiql, 17-Hinth

Hapa kuna maelezo kuhusu saba iliyobaki:

11-Munkar: Neno hili linatokana na mzizi wa neno Inkar lenye maana ya isiyojulikana. Dhambi haiendani na Fitra (maumbile asili) na akili na hivyo katika maumbile asili ya mwandamu ni jambo  lisilojulikana na mbaya. Neno Munkar limetumika mara 16 katika Qur'ani Tukufu, hasa katika maneno Nahy anil Munkar (kuzuia maovu).

12 -Fahisha: Maana yake ni neno au kitendo ambacho ubaya wake hauna shaka. Neno hilo hutumika kurejelea vitendo viovu na vya kufedhehesha sana. Imetumika mara 24 kwenye Qur'ani Tukufu.

13-Khibth: Inahusu kitu chochote kichafu na cha kuchukiza na ni kinyume cha Tayyib, ambayo ina maana safi na ya kupendeza. Neno Khibth limetumika mara 16 kwenye Qur'ani Tukufu.

14-Shar: Shar au shari maana yake ni kitendo chochote kiovu ambacho watu wanachukia na na kinyume chake ni Khayr au kheri, maana yake kile ambacho watu wanakipenda. Shar inatumika zaidi juu ya majanga na shida lakini pia juu ya dhambi. Neno hilo limetumika katika aya kadhaa za Qur'ani Tukufu ikiwa ni, pamoja na Aya ya 8 ya Surah Al-Zilzal.

15-Lamam: Lamam inamaanisha kukaribia dhambi na pia inamaanisha vitu vidogo. Inatumika kurejelea dhambi ndogo (Saghira). Neno hilo limetumika mara 26 katika Qur'ani Tukufu.

16- Wizr: Wizr ina maana ya uzito na inatumika kurejelea kubeba dhambi za wengine. Imetumika mara 26 katika Qur'ani Tukufu.

Wakati mwingine neno Thiql pia hutumika kumaanisha uzito wa dhambi, ikiwa ni pamoja na katika Aya ya 13 ya Surah Al-Ankabut.

17-Hinth: Hinth maana yake ni mwelekeo wa uwongo na mara nyingi hutumika kurejelea kuvunja ahadi. Neno hili limetumika mara mbili katika Qur'ani Tukufu..

Maneno haya 17 kila moja yanarejelea kipengele kimoja cha matokeo ya kutisha ya dhambi na yana onyo

Kishikizo: qurani tukufu dhambi
captcha