IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu hivi sasa ni zaidi ya baada 9/11

13:04 - November 15, 2023
Habari ID: 3477894
OTTAWA (IQNA) - Mwanaharakati wa Kiislamu wa Kanada (Canada) alielezea kiwango cha chuki dhidi ya Uislamu na ukandamizaji Waislamu nchini humo katika wiki za hivi karibuni kuwa haujawahi kutokea.

Katika takriban miaka 30 kama mwanzilishi mwenza na rais wa wakati huo wa Jukwaa la Waislamu wa Kanada, Samer Majzoub alisema hajawahi kuona kiwango cha uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu na vitisho vilivyoripotiwa tangu Oktoba 7.

"Kusema kweli, haijaongezeka tu, imepindukia," Majzoub alisema Jumatatu. “Imevuka kiwango tulichoona baada ya mashambulizi ya 9/11. Na tunaona aina mpya za unyanyasaji dhidi ya Uislamu."

Watu wamepiga simu kuripoti vitisho katika maeneo yao ya kazi, shuleni na vyuo vikuu. Vitisho hivyo ni pamoja na madereva kuwatemea mate watu kutoka kwenye madirisha ya gari na watu binafsi kusukumwa au kutukanwa. Matukio yanaripotiwa kote Kanada, na polisi wa Montreal wamehesabu idadi inayoongezeka ya uhalifu unaohusiana na chuki dhidi ya shabaha za Kiislamu na Kiyahudi katika mwezi uliopita.

Mwishoni mwa Oktoba, msikiti katika Kituo cha Kiislamu cha Badr huko St-Léonard ulichorwa alama ya swastika na ujumbe wa "Ueni wote (Waislamu)".

Ijumaa na Jumamosi iliyopita, Jukwaa la Waislamu wa Kanada lilipokea ripoti za wanawake Waislamu kushambuliwa kwa maneno karibu na misikiti.

"Hawa walikuwa wanawake wachanga tu. Walikuwa wanafunzi,” Majzoub alisema.

Idadi ya kweli ni kubwa zaidi kwa sababu wananchi wengi wanasitasita kuandikisha ripoti kwa hofu ya vitisho au kulipizwa kisasi, au kwamba malalamiko yao hayatachukuliwa kwa uzito na polisi, kama ilivyoripotiwa hapo awali. Hivi majuzi, hata hivyo, Majzoub alisema jeshi la polisi la Montreal limekuwa likifanya mawasiliano na watu wa jamii ya Kiislamu.

Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Kanada limerekodi ongezeko la asilimia 1,300 la idadi ya matukio ya chuki yaliyoripotiwa tangu Oktoba 7, alisema Fatema Abdalla, afisa wa utetezi katika shirika hilo. Baraza limepokea wastani wa malalamiko manane kwa siku kote Kanada, huku matukio mengi yakitokea katika maeneo yenye watu wengi huko Ontario, Alberta na Quebec.

3486010

captcha