IQNA

Wiki ya Umoja wa Kiislamu

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran asisisitiza ulazima wa kuweko umoja baina ya Waislamu

17:22 - September 29, 2023
Habari ID: 3477666
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa jijini Tehran amesisitiza umuhimu wa umoja wa Waislamu huku Waislamu wakiadhimisha 'Wiki ya Umoja wa Kiislamu' duniani kote.

Hujjat-ul-Islam wal-Muslimeen Kadhim Siddiqui Imam muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza ulazima wa kuweko umoja baina ya Waislamu.

Akihutubu katika Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran amesema: "Shetani ni miongoni mwa vyanzo vya kuvuruga umoja, na Qur'ani Tukufu inamtambulisha Shetani kuwa ndiye chanzo cha mifarakano na migongano. Katika dunia ya leo, shetani mkuu ni Marekani akishirikiana na Uingereza ambayo  chanzo cha uovu."

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Hujjatul Islam Siddiqui amegusia hotuba ya hivi karibuni ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Seyed Ebrahim Raisi katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo aliitaja Qur'ani Tukufu kuwa ni kitabu chenye kujenga ustaarabu na binadamu na chimbuko la umoja na kusema: Raiswa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameiarifisha Qur'ani katika Umoja wa Mataifa kama kama chanzo cha nuru."

Inafaa kuashiria hapa kuwa, tuko katika siku tukufu za kuadhimisha Maulid ya Mtume Mtukufu wa Uislamu Mohammad al Mustafa SAW, siku ambazo ni maarufu kama siku za Maulidi. Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaadhimisha siku hiyo tarehe 12 Rabiul Awwal na Waislamu wa Madhehebu ya Shia wanamini siku hiyo ni tarehe 17 Rabiul Awwal.

Miaka mingi iliyopita, Hayati Imam Khomeini MA, Kiongozi mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye binafsi alikuwa mstari wa mbele kulingania umoja wa Kiislamu alipendekeza kuwa, muda uliopo baina ya tarehe hizo mbili uwe ni "Wiki ya Umoja wa Waislamu" kwa lengo la kuimarisha mashikamano na udugu baina ya madhehebu za Kiislamu.

4171882

Habari zinazohusiana
captcha