IQNA

Mameya Canada wataka kikao kujadili ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu

15:09 - June 26, 2021
Habari ID: 3474044
TEHRAN (IQNA) - Mameya wa miji miwili ya Canada ambayo imeshuhudiwa hujuma dhidi ya Waislamu wamemtumia barua waziri mkuu Justin Trudeau wakitaka kuitishwe kikao cha kujadili chuki dhidi ya Uislamu.

Katika barua zao, Meya wa London Ed Holder na Meya wa Quebec Regis Labeaume amelisifu bunge kwa kuidhinisha Kikao cha Kitaifa cha Dharura Kuhusu Chuki Dhidi ya Uislamu (Islamophobia) lakini wamesmea kikao hicho kinapaswa kuitishwa haraka iwezekanavyo.

Barua hiyo imekuja baad aya Waislamu wanne wa fmailia moja kuuawa baada ya lori kwagonga kwa makusudi katika mji wa London. 

Waliouawa katika shambulizi hilo la Juni sita ni baba wa familia, Salman Afzal, 46; mke wake Madiha, 44; binti yao Yumna, 15; na bibi aliyekuwa na umri wa miaka 74 ambaye jina lake limehifadhiwa. Mtoto mdogo wa kiume wa familia hiyo, Fayez, 9, alijeruhiwa vibaya na amelazwa hospitalini.

Kijana mwenye umri wa miaka 20, Nathaniel Veltman, aliyetekeleza unyama huo amefunguliwa mashitaka manne ya kuua kwa makusudi, na shitaka moja la jaribio la kuua. Polisi ya Canada inasema chuki za kidini ndiyo sababu ya hujuma hiyo.

Aidha Januari 2017, Waislamu sita – Aboubaker Thabti, Abdelkrim Hassane, Khaled Belkacemi, Mamadou Tanou Barry, Ibrahima Barry na Azzedine Soufiane – waliuawa wakati Bissonnette alipofyatua risasi ndani ya Kituo cha Kiislamu cha mji wa Quebec.

Mameya hao wanataka kikao hicho kiitishwe ili kujadili njia za kuzuia mashambulizi dhidi ya Waislamu ili watu wa jamii zote Canada waishi kwa amani na maelewano.

3475049

captcha