IQNA

Aliyewaua Waislamu Canada akabiliwa na shtaka la ugaidi

21:43 - June 15, 2021
Habari ID: 3474008
TEHRAN (IQNA)- Raia wa Canada aliiyeua Waislamu wanne wa familia moja kwa sababu tu ya dini yao amesomewa tuhuma za muaji ya daraja la kwanza na kufanya ugaidi.

Wendesha mashtaka wa mkoa na Federesheni ya Canada usiku wa kuamkia Jumatatu waliidhinisha kufunguliwa mashtaka Nathaniel Veltman kwa tuhuma za mauaji ya makusudi.

Mauaji hayo ya familia ya Kiislamu pia yametambuliwa kuwa ni hujuma ya kigaidi.

Jumapili iliyopita, kijana huyo mwenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu (20) aliua watu wanne wa familia moja na kujeruhi vibaya mwingine, baada ya kuwagonga kwa makusudi na lori lake katika mkoa wa Ontario. Ushahidi unaonesha kuwa hatua hiyo ya kigaidi ilipangwa tangu hapo awali na halikuwa tukio la sadfa.

Waliouawa katika shambulizi hilo wametajwa kuwa ni baba wa familia, Salman Afzal, 46; mke wake Madiha, 44; binti yao Yumna, 15; na bibi aliyekuwa na umri wa miaka 74 ambaye jina lake limehifadhiwa. Mtoto mdogo wa kiume wa familia hiyo, Fayez, 9, amejeruhiwa vibaya na amelazwa hospitalini.

Takwimu zilizotolewa na Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Canada zinaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 kumefanyika hujuma na mashambulizi 300 dhidi ya Waislamu nchini humo na kwamba, zaidi ya mashambulizi 30 yaliambatana na ukatili mkubwa. 

3977566

Kishikizo: waislamu canada
captcha