IQNA

Maulamaa wa Kiislamu Afrika Mashariki watangaza vita dhidi ya Uwahabi, misimamo mikali

6:00 - August 30, 2015
Habari ID: 3353847
Zaidi ya maulamaa na maimamu 300 wa Kiislamu Somalia, Kenya, Tanzania, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametangaza Fatwa ya kupambana na kundi la kigaidi la al-Shabab na itikadi yenye misimamo mikali ya Uwahhabi.

Kwa mujibu wa gazeti la Standard linalochapishwa nchini Kenya, maulamaa hao wamesema kuanzia sasa watajiunga na serikali za nchi zao katika kuangamiza misimamo mikali. Aidha wameonya kuwa misimamo mikali ya kidini ni tishio kwa nchi huru na uchumi wa nchi hizo.
Baada ya kongamano la siku mbili liliofanyika katika mji wa Mackinnon Road  Kaunti ya Kwale eneo la Pwani, maualmaa hao kutoka Tarika mbali mbali za Kisuni wamesema makundi ya yanayojiita ya Kisalafi, ambapo kundi la kigaidi la al Shabab zinafuata makundi hayo, chimbuko lake ni itikadi potofu ya Kiwahhabi ambayo imeuteka Uislamu.
Mulamaa hao waliokutana  Jumapili na Jumatatu iliyopita katika kituo cha Al Mahmudiyah Sufi Islamic Centre ingawa Usufi unasisitiza kustahamiliana na misimamo ya wastani, walipuuza nguvu za itikadi za Kiwahhabi na makundi ya Kisalafi.

Katika kongamano hilo, kulisisitizwa pia udharura wa kushirikiana na serikali za nchi husika kwa ajili ya kuyashinda makundi hayo ya Kiwahabi hususan al-Shabab. Maulama hao pia wametahadharisha kuhusu njama na hatari za  makundi hayo ya kufurutu ada ya kujinasibisha na dini kutokana na kuathiri uchumi wa nchi za Kiafrika. Wamesema kuwa makundi ya Kisalafi, kama lile la al-Shabab, Boko Haram, Daesh na mengine, yanaathiriwa na mafundisho ya Kiwahabi na kwamba yamepora Uislamu. Wanazuoni hao wamelaani njama za kuwagawa Waislamu na wasiokuwa Waislamu zinazofanywa na makundi hayo na kuongeza kuwa, kwa miaka mingi Waislamu wa Afrika Mashariki wa madhehebu tofauti wamekuwa wakishirikiana katika shughuli zote za kimaendeleo na kwamba, umefika wakati wa kukabiliana na wimbi la makundi hayo yenye uelewa potofu wa dini ya Kiislamu.../mh.

3353455

captcha