IQNA

OIC yataka watalwa wa Israel washtakiwe kwa kutenda jinai

20:53 - September 28, 2014
Habari ID: 1455018
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetaka washtakiwe wakuu wa kijeshi na kisiasa wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu.

Iyad Amin al Madani Katibu Mkuu wa OIC ameikosoa Israel kwa kuwafanyia Wapalestina vitendo visivyo vya kibinadamu kwa miongo kadhaa sasa. Amesema kuwa, kuna kesi kubwa ya kuitaja Israel kuwa ni utawala wa ‘ubaguzi wa rangi’ ambao unapaswa kushughulikiwa kimataifa. Al Madani ameongeza kuwa, wamekuwa wakifanya majadiliano ya kuishauri serikali ya Palestina kujiunga na Mkataba unaounda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na kuwa mwanachama wa korti hiyo. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu pia amesema, OIC inaunga mkono mpango wa Palestina wa kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liainishe muda wa kuondoka Israel katika ardhi inazozikalia kwa mabavu za Palestina.../mh

1454923

Kishikizo: oic israel palestina iyad
captcha