IQNA

OIC kuunga mkono ombi la Palestina UN

10:13 - April 06, 2014
Habari ID: 1390963
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imesema itaunga mkono ombi la Palestina kwa Umoja wa Mataifa kujiunga na na mikataba 15 ya kimataifa.

Iyyad Amin Madani  Katibu Mkuu wa OIC  amesema jumuiya hiyo inaunga mkono kikamilifu juhudi za Palestina kijiunga na mikataba hiyo ya kimataifa. Aidha amukosoa vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina.
Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulisema kuwa umepokea barua za Wapalestina kwa ajili ya kujiunga na mikataba 13 ya kimataifa. Naibu msemaji wa umoja huo Farhan Haq amethibitisha kupokewa barua hizo za maombi na kusema kwamba hatua za kiofisi zitakapokamilika watazijadili ili kujua hatua zinazofuata. Miongoni mwa mikataba ya kimataifa Wapalestina wanayotaka kujiunga nayo ni Mkataba wa Vienna wa Uhusiano wa Kimataifa, Mkataba wa Haki za Watoto, mkataba wa kuzuia Aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na Mkataba wa Haki za Kiraia na Kisiasa. Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa, wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya Israel kushindwa kutekeleza ahadi zake ikiwa ni pamoja na kuwaachia huru mateka wa Palestina. Maafisa wa Palestina walikubaliana kuacha kufuatilia mpango wa kujiunga na taasisi za kimataifa na kuishitaki Israel wakati mazungumzo ya upatanishi na utawala huo ghasibu yakiendelea na badala yake Tel Aviv iwaachie huru mateka 103 wa Palestina.
1390881

Kishikizo: palestina israel MADANI oic
captcha