iqna

IQNA

imam
Qur'ani Tukufu Inasemaje /40
TEHRAN (IQNA) – Kuna nafasi tatu ambazo kila Mtume wa Mwenyezi Mungu amepewa angalau moja kati ya hizo na utume unaotokana na nafasi hiyo.
Habari ID: 3476236    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/12

Wafanyaziara takribani milioni 27 wakiwemo wageni milioni tano wameshiriki katika maombolezo ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW, Imam Hussein AS, katika mji wa Karbala nchini Iraq.
Habari ID: 3459722    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/04

Waislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia leo wamehuisha kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein AS, mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW huku watu milioni 26 wakiripotiwa kufika Karbala, Iraq hadi sasa kwa ajili ya maombolezo hayo.
Habari ID: 3459439    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/02

Takribani miaka 1376 iliyopita, ilifanyika majlisi ya kwanza ya siku ya Arubaini tangu kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW Imam Hussein bin Ali AS akiwa na watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume ambao waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria.
Habari ID: 3459320    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/02

Karibu watu milioni moja wameshiriki katika msafara wa kutembea kwa miguu kutoka mji wa Kaduna hadi Zaria kwa mnasaba wa Arubaini ya Imam Hussein AS katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria.
Habari ID: 3459300    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/01

Kiongozi Muadhamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema harakati iliyojaa mahaba na imani ya watu wa nchi mbali mbali za dunia katika siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS ni moja kati ya ishara za Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3458796    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/30

Kundi la kigaidi Boko Haram limetangaza kuhusika na shambulio dhidi ya msafara wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia waliokuwa katika msafara wa maombolezo ya Imam Hussein AS jimbo la Kaduna nchini Nigeria.
Habari ID: 3458202    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/29

Warsha ya kuhusu kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein AS imefanyika Bauchi nchini Nigeria.
Habari ID: 3454535    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/19

Professor Abdulaziz Sachedina
Kila ambaye anatafakari kuhusu msingi wa kimaanawi wa uwepo wa mwanadamu na ujumbe wa Qur'ani kuhusu umaanawi katika zama zetu hizi, anapaswa kusoma aliyoyasema Imam Khomeini MA kuhusu Qur'ani Tukufu
Habari ID: 3428266    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/01

Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu Iran Ayatullah Hashemi Rafsanjani amesema kuwa Qur'ani tukufu ilikuwa chanzo cha shakhsia na mafanikio makubwa ya hayati mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini MA.
Habari ID: 3428213    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/01

Idara ya Qur’ani katika Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran imeandaa kongamano chini ya anuani ya ‘‘Qur’ani Katika Sirah na Fikra za Imam Khomeini’.
Habari ID: 3410354    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/29

Ashura ni tukio ambalo imepita miaka takribani 1375 tokea kujiri kwake lakini si tu kuwa tukio hili la kihistoria linawavutia Waislamu bali pia wapenda uhuru kote duniani wamevutiwa na yaliyojiri katika jangwa la Karbala.
Habari ID: 3392955    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/23

Idara ya waqfu iliyo chini ya Wizara ya Waqfu nchini Misri, imeamuru kufungwa msikiti wa Imamul-Hussein (as) mjini Cairo kuanzia jana Alkhamis hadi baada ya kesho Jumamosi ikiwa ni katika kuwazuia Waislamu wa Kishia kutekeleza marasimu za Taasua na Ashura.
Habari ID: 3392920    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/23

Tuko katika mwezi wa Muharram ambao unahuisha na kurejesha akilini kumbukumbu ya mapambano adhimu na yenye adhama. Muharram ni mwezi uliofungamana na jina la Hussein Ibn Ali (AS) na harakati isiyo na mbadala ya mtukufu huyo katika ardhi ya Karbala.
Habari ID: 3391638    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/22

Katika jitihada za kuleta umoja baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, kumefanyika Majlisi za maombolezo Mwezi wa Muharram katika msikiti wa Masunni ambapo khatibu alikuwa ni mwanazuoni wa Kishia katika Kituo cha Kiislamu cha Dearborn, Michigan nchini Marekani.
Habari ID: 3391260    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/21

Waislamu watano wa madhehebu ya Shia wameuawa nchini Saudi Arabia kufuatia hujuma ya kundi la kigaidi la Daesh au ISIS katika majlisi ya maombolezo ya siku 10 za Muharram.
Habari ID: 3386096    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/17

Siku ya Alkhamisi ya tarehe 4 Juni inasadifiana na kumbukumbu za siku ya kufariki dunia Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3310852    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/04

Siku ya 15 ya mwezi mtukufu wa Shaaban ni siku ya kuzaliwa Mtukufu Imam wa Zama Imam Mahadi (-Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake-af).
Habari ID: 3310767    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/03

Kongamano la 11 la Kimataifa la Itikadi ya Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) limeanza Jumapili hii hapa mjini Tehran na kushirikisha pamoja shakhsia mbalimbali wa ndani na nje ya Iran
Habari ID: 3309948    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/01

Takribani watu milioni 20 wamewasili Karbala kwa ajili ya kushiriki katika Arubaini ya Imam Husain AS. Mkuu huyo wa mkoa wa Karbala amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kabisa kumiminika watu kiasi chote hicho katika historia ya ziara za Imam Husain AS.
Habari ID: 2617895    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/13