Hujjatul Islam Seyed Mohammad Zolfaqari, mkurugenzi wa idara ya wafanya ziara wasio Wairani ya Astan Quds Razavi (Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ridha AS) , aliiambia IQNA kwamba watoto 40 na vijana kutoka nchi 12 wamehudhuria sherehe hiyo.
Hafla hiyo imefanyika katika Rawaq zote (nafasi zenye paa zilizounganishwa na Haram tukufu), alibainisha.
Kwa mujibu wa mwanazuoni huyo, hafla hiyo inawashirikisha watoto na vijana wakiimba qasida za kuwasifu Ahl-ul-Bayt (AS), na kuwapongeza Waislamu kwa kuwasili kwa Ramadhani na kuwakumbusha watu baraka za mwezi huu mtukufu.
Amesema ibada hiyo inafanyika katika madhabahu tukufu ya Imam Reza (AS) kwa mwaka wa pili mfululizo kwa lengo la kuziweka hai mila hizo njema na kuchangia katika kusambaza thamani za Kiislamu kwa vizazi vijavyo.
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ulianza Jumatatu katika baadhi ya maeneo ya dunia na Jumanne katika maeneo mengine kwa kutegemea mwezi mwandamo.
3487520