Hii ni kwa sababu mtu anapoamua kulipa kile anachotakiwa kulipa kidini, kama vile Khums, Shetani humuonya kuhusu kutumbukia katika umasikini akifanya hivyo. “ Shet'ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.” (Aya ya 268 ya Surah Al-Baqarah)
Lakini Mwenyezi Mungu anaapa katika Qur'ani Tukufu kwamba ataifidia:
“Sema: Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakacho kitoa Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanao ruzuku.” (Aya ya 39 ya Surah Saba)
“ Na shikeni Sala na toeni Zaka; na kheri mtakazo jitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yafanya..” (Aya ya 110 ya Surat Al-Baqarah
“Watoto na mali ni pambo la maisha ya dunia, lakini kwa matendo yanayoendelea kuzalisha wema mtu anaweza kupata malipo bora kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuwa na matumaini makubwa Kwake.” (Aya ya 46 ya Surah Al-Kahf)
" Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini." (Aya ya 96 ya Surah An-Nahl)
“Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua." (Aya ya 261 ya Surah Al-Baqarah)
Iwapo Shetani atashindwa kumsadikisha mtu kukwepa kulipa Khums, atajaribu kumshawishi kuiahirisha, akisema: Naam, ndiyo, kulipa Khums ni Wajib (wajibu), lakini huna haja ya kufanya haraka. Namna gani ikiwa unakabiliwa na tatizo la kifedha? Je, ikiwa utapata hasara? Je kama…?
Qur'ani Tukufu inaonya dhidi ya ucheleweshaji kama huo: