IQNA

Fikra

'Serikali Kibaraka': Jinsi mwanafalsafa mashuhuri Mwislamu aliiona Israel miaka 60 Iliyopita

22:41 - November 17, 2023
Habari ID: 3477905
TEHRAN (IQNA) – Wanafalsafa na wanafikra wa Kiislamu pia wamekuwa wakitilia maanani maendeleo ya ummah Kiislamu pamoja na kujihusisha na fikra za kina za kifalsafa.

Seyyed Mohammad Hussein Tabatabai (1904-1981 CE), anayejulikana zaidi kama Allamah Tabatabai, alikuwa miongoni mwa wanafikra hao ambao hawakuweza kukaa kimya mbele ya tishio lililojitokeza dhidi ya mataifa ya Kiislamu.

Mbali na kufundisha katika vyuo vya Kiislamu au Hauzah, Allamah Tabatabai pia alikuwa akitoa majibu kwa wanafunzi kutoka kote ulimwenguni ambao wangeuliza kuhusu masuala mbalimbali kupitia barua.

Baadhi ya maswali yalihusu utaalamu wake mkuu; Falsafa ya Kiislamu, nyanja ambayo inashughulikia maswali ya kimsingi kuhusu kuwepo, ikiwa ni pamoja na mada kama vile sababu, maarifa, nafsi, Mwenyezi Mungu, na dini, kwa kutumia mbinu ya kimantiki na ya mjadala.

Wakati huo huo, kulikuwa na barua ambazo zilirejelea masuala ya kisasa. Mwaka 1963 mwanafunzi aliyekuwa akiishi Marekani aliuliza swali kuhusu kuanzishwa kwa taifa la Kiyahudi yaani utawala haramu wa Israel katika ardhi ya Palestina.

Swali lilirejelea baadhi ya riwaya zilizosema Mayahudi wasingeweza kuanzisha nchi huru. Mwanafunzi huyo alidai kwamba  kuanzishwa “Israeli” kulithibitisha kuwa riwaya ilikuwa si sahihi. Mwanafunzi aliuliza iwapo riwaya au hadhithi kama hizo ziliibuliwa kwa akili ya kuleta uadui kati ya watu wa eneo.

Kujibu, Allamah Tabatabi anaandika:

Huko Palestina, kuna sehemu ndogo ambayo hutumika kama bandari na kituo cha kijeshi cha Waingereza, Wafaransa, na Wamarekani, na serikali ya vibaraka inayojulikana kama serikali ya Israeli inadhibiti eneo hili. Licha ya kuwepo kwake kwa muda mfupi, serikali hii imejitolea kwa juhudi kubwa kuimarisha na kuandaa eneo hilo kwa kadiri inavyowezekana. Zaidi ya hayo, wametumia ushawishi mkubwa sana kuzuia mataifa ya Kiislamu kuungana dhidi yao.

Akibainisha kwamba kulikuwa na baadhi ya sera duniani zinazotaka kudumisha ujinga na chuki dhidi ya Uislamu, alirejea pia baadhi ya marejeo ya Qur'ani Tukufu  kuhus  Mayahudi:

Baada ya kutaja jinai za Mayahudi na khiana zao dhidi ya Uislamu na Waislamu, na baada ya kuwausia Waislamu kuwa wamoja na kuzishika sheria za kidini na wasiwe na urafiki na Mayahudi wala kuwatiii, Qur’ani Tukufu inasema hasira ya Mwenyezi Mungu iko juu ya Mayahudi, na wameangamia. kudhalilishwa na kufedheheshwa milele na hawawezi kuwadhuru Waislamu, isipokuwa Waislamu wawaruhusu kufanya hivyo, kwa kumuasi Mwenyezi Mungu na sheria zake. [Surah Al-Imran]

Katika aya nyingine, Qur’ani Tukufu inaelekeza kwenye sababu ambayo inaweza kuruhusu jambo hilo kutokea ni kuwachukua Wayahudi kama washirika, alisema Allamah Tabatabai.

"Kama unavyoona, Mwenyezi Mungu anaahidi ustawi wa Uislamu mkabala wa Uyahudi kwa Waislamu ikiwa Waislamu watafuata sheria za Kiislamu na kudumisha umoja. Ustawi huu sio kwa nchi za Kiislamu ambazo hazina chochote isipokuwa jina la Uislamu," aliongeza katika barua hiyo, iliyoandikwa awali  kwa Kifarsi.

Allamah Tabatabai alionya dhidi ya muungano wa baadhi ya Waislamu na utawala wa Israel miongo sita iliyopita lakini watawala wa baadhi ya nchi zenye Waislamu wengi kama vile Misri, Jordan, Bahrain, UAE, na Morocco wana uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel

Allamah Tabatabi ni nani?

Allamah Tabatabai alikuwa mwanazuoni mashuhuri wa Iran, mwanafalsafa, na mwanafikra wa Uislamu wa kisasa wa madhehebu ya  Shia. Alizaliwa mnamo 1903 huko Tabriz na alikufa mnamo 1981 huko Qom.

Alisoma huko Najaf, Iraq, ambapo alibobea katika nyanja mbalimbali za sayansi ya Kiislamu, kama vile tafsir, fiqh, hadithi, kalam na falsafa. Pia alijifunza kutoka kwa wanazuoni  mashuhuri, kama vile Ali Tabatabai, Mirza Muhammad Husain Na'ini, na Sayyid Abu'l-Qasim Khwansari.

Aliandika vitabu na makala nyingi juu ya mada tofauti, kuhusu tafsiri ya Qur’ani Tukufu, falsafa, irfani, historia, na maadili. Kazi yake maarufu zaidi ni Tafsir ya Qur’ani Tukufu ya al-Mizan, ambayo ina juzuu 27 na ambayo aliandika kati ya 1954 na 1972.

Pia aliandika Kanuni za Falsafa na Mbinu ya Uhalisia, kazi yenye juzuu tano kuhusu falsafa ya Kiislamu, yenye maelezo ya Ustadh Murtadha Mutahari. Pia alikuwa na midahalo na Henry Corbin, mwanafalsafa wa Ufaransa na mtaalam wa masuala ya mashariki, kuhusu masuala mbalimbali ya fikra za Kiislamu.

Alichukua nafasi kubwa katika uamsho wa kiakili katika vyuo vya Kiislamu katika mji  Qom nchini Iran na ukuzaji wa falsafa ya Kiislamu, tawi ambalo lilianzishwa na Abu Nasr Muhammad al-Farabi (870-950 CE) na lina fikra  kuu tatu ambazo ni: falsafa ya Peripatetic au "Mashsha, falsafa ya Illuminationist au "Ishraq", na falsafa ya "al-Hikmat al-Muta'aliya".

captcha