IQNA

Vikosi vya Israel kuwafukuza waumini wa Kiislamu katika Msikiti wa al-Aqsa

11:21 - June 21, 2023
Habari ID: 3477175
Vikosi vya Israel vimeripotiwa kuwafukuza waumini wa Kiislamu katika Msikiti wa al-Aqsa ili kujiandaa na uvamizi haramu wa walowezi wa Israel.

Jana usiku, polisi wa utawala ghasibu wa Israel walivamia Msikiti wa Al-Aqsa, eneo la tatu la Utukufu  katika Uislamu, lililoko katika Mji Mkongwe wa al-Quds, na kuwatimua kila mtu ndani, wakiwemo wafanyakazi wa Waqf na waumini wa usiku, mashahidi walisema. Walisema polisi walifunga milango yote ya boma la Utukufu  na kuwazuia watu kuingia humo bila kutoa sababu yoyote ya kitendo chao, Shirika la Habari la Wafa lilitoa Taarifa;  Waumini hao wa kike wa kuabudu usiku waliamua kuendelea na mkesha wao kwenye ngazi za Lango la Damascus, lango kuu la kuingilia Mji Mkongwe wa Jerusalem, kupinga hatua ya polisi kabla ya wao pia kulazimishwa kuondoka eneo hilo na polisi. Hatua hiyo ya polisi inaaminika kuwa inahusiana na kuwaondoa Waislamu katika jumba Tukufu  la waumini wa Kipalestina wakati Wayahudi wenye itikadi kali wanaanza uvamizi wa asubuhi ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa. Milango ya Msikiti wa Al-Aqsa ilifunguliwa baadaye lakini watu wazee tu ndio walioruhusiwa kuingia. Asubuhi ya leo, makumi ya wafuasi wa itikadi kali za Kiyahudi na walowezi walivamia Msikiti wa Al-Aqsa na kuzunguka katika nyaya  zake, baadhi yao  wakifanya ibada za Kiyahudi kinyume na hali ilivyo sasa,  yanayosemwa kuwa Waislamu pekee ndio wanaoweza kuswali katika boma hilo lililozungushiwa ukuta. Kwa kawaida Waislamu husali usiku na mchana katika Msikiti wa Al-Aqsa katika siku 10 za mwanzo za mwezi wa Dhu al-Hijja, ambao hufikia mwisho tarehe 10 ya mwezi kwa kuhiji huko Makka.

 

3484020

captcha