IQNA

Ukombozi wa Palestina

Harakati ya Jihad ya Kiislamu kulipiza kisasi mauaji ya Israel kwa wanachama wake

16:58 - May 25, 2023
Habari ID: 3477044
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu (Jihad Islami) ya Palestina alisema harakati hiyo italipiza kisasi kwa mauaji ya wanachama wake kwa kuishambulia Tel Aviv kwa moto.

Katibu Mkuu wa Jihad ya Kiislamu Ziad al-Nakhala alisema katika mahojiano yake yaliyochapishwa Jumatano kwamba makundi yote ya muqawama ya Kiislamu yangeingia katika vita dhidi ya utawala wa haramu wa Israel kama ingeendeleza uchokozi wake wa hivi punde dhidi ya Ukanda wa Gaza.

"Kama vita vya hivi majuzi vingeendelea, makundi yote ya muqawama, ikiwa ni pamoja na Hamas (kundi la mapambano ya Kiislamu Palestina lenye makao makuu ya Gaza) na Hizbullah [ya Lebanon], yangeanza kuchukua hatua," alisema.

Utawala haramu wa Israel ulianzisha kampeni ya mashambulizi mabaya ya mabomu dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Mei 9, na kuua makumi ya Wapalestina, wakiwemo makamanda watano wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu. Kundi hilo la Jihad Islami lilijibu kwa kurusha zaidi ya roketi 1,000 kuelekea Israeli.

Mgogoro huo uliashiria tukio baya zaidi la mapigano kati ya makundi ya upinzani ya Gaza na utawala wa Israel tangu vita vya siku 10 vilivyowekwa na Tel Aviv kwenye eneo la pwani lililozingirwa mwaka 2021.

Pande hizo mbili zilikubaliana kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Misri baada ya siku tano za mapigano. Nakhala alilitaja kundi la Jihad Islami kuwa ndilo kundi lililochukua sehemu kubwa zaidi ya jukumu la kuupiga vita utawala wa Israel wakati wa vita hivyo na kusema kuwa, muqawama huo utalipiza kisasi kwa mauaji ya wanachama wake kwa kuishambulia Tel Aviv kwa moto.

Kiongozi huyo wa muqawama aliendelea kwa kudai kuwa haukuwa upinzani, ambao ulishinikizwa kusitisha kulipiza kisasi wakati wa vita.

"Badala yake ilikuwa ni hesabu za adui, zikielekeza kwenye [uwezekano] wa kuingilia vita kwa makundi [nyingine] ya Wapalestina na Hizbullah, ambayo iliifanya Tel Aviv kuacha kuzidisha uchokozi wake."

3483696

captcha