IQNA

Taarifa ya ISESCO

Maonyesho ya Seerah ya Mtume Muhammad SAW huko Rabat yarefushwa kwa miezi sita zaidi

21:57 - April 28, 2023
Habari ID: 3476929
TEHRAN (IQNA) - Shirika la Nchi za Kiislamu la Utamaduni, Elimu na Sayansi (ICESCO) lilitangaza kurefushwa muda wa Maonyesho ya Kimataifa ya Seerah ya Mtume Muhammad SAW na Ustaarabu wa Kiisilamu katika makao makuu yake huko Rabat, Moroko, kwa miezi mingine sita.

Kwa msingi huo, maonyesho hayo yataendelea kwa muda wa mwaka moja katika makao makuu ya ISESCO. Maonyesho hayo yalizinduliwa Novemba 17, 2022, tovuti ya ISESCO iliripoti.

Hii ni mara ya kwanza kwa maonyeso hayo kufanyika nje ya Saudi Arabia kwani yameuwa yakifanyika katika mji wa Madina Al Munawarah.

Tangu ufunguzi wake wa umma mnamo Novemba 28, 2022, maonyesho hayo yamevutia wageni karibu milioni moja na nusu, kutoka wakiemo raia wa Moroko na wageni wa kimataifa.

Wasomi na wanafikra maarufu kutoka ulimwengu wa Kiisilamu wametembelea maonyesho hayo ambayo ni marejeo muhimu kwa wale wanaotaka kuongeza uelewa wao juu ya wasifu na mafundisho ya Nabii Muhammad (PBUH).

Maonyesho yanalenga kufikisha ujumbe wa Uislamu na maadili yake ya haki, amani, rehema, uvumilivu, umoja na misimamo ya wastani, yote ambayo yameingizwa sana katika Qur’ani Tukufu, Sunnah ya Mtume SAW na historia ya Uislamu.

captcha