IQNA

Mfumo wa Fedha wa Kiislamu

Shirika la Kiislamu la kuuza hisa lazinduliwa Tanzania

12:18 - March 06, 2023
Habari ID: 3476665
TEHRAN (IQNA)- Kampuni mpya ilizinduliwa nchini Tanzania ili kushughulikia udalali wa Hatifungani (Dhamana za muda mrefu) Kiislamu na kutoa huduma za ushauri wa uwekezaji kuhusiana na bidhaa zinazotii sheria za Kiislamu

Kampuni hiyo inayojulikana kama Yusra Sukuk Company Ltd, ni kampuni ya kwanza ya udalali ya Kiislamu nchini Tanzania na eneo zima laAfrika iliyo kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa mujibu wa mwenyekiti wake, Mohammed Issa.

"Kampuni yetu ina leseni mbili za kushughulika dhamana na kufanya kazi kama mshauri wa uwekezaji," Bw Issa alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.

"Jambo moja muhimu ni kwamba Yusra Sukuk hashindani na kampuni katika tasnia lakini inalenga kuharakisha ukuaji wa sekta kwa kushirikiana na wahusika wengine," alisema na kuongeza kuwa itashughulika tu na biashara zinazofuata sheria za Kiislamuna kutoa mwanya kwa uwekezaji wa Halal.

Ingawa shirika hilo linafuata vigezo vya Kiislamu katika huduma zake, lakini  atu wote bila kujali tofauti za kidini anaweza kupata huduma hizo.

Kampuni hiyo imekuja wakati ambapo Tanzania imeshuhudia ongezeko la utoaji wa huduma za kifedha za Kiislamu, zinazohitaji washauri wa kitaalamu.

Hivi sasa, Tanzania ina benki moja tu yenye mamlaka kamili, Amana Bank, ambayo inatoa huduma za kifedha kwa kufuata sheria za Kiislamu huku kukiwa na benki kadhaa za kawaida lakini zenye kitengo cha huduma za benki za Kiislamu.

Mwaka jana  Benki ya KCB Tanzania ilizindua Hatifungani (Dhamana za muda mrefu) yake ya kwanza ya Kiislamu yenye thamani ya Tsh10 bilioni ($4.4 milioni) kufadhili kitengo cha Sahl cha benki hiyo.

Hatifungani hiyo ya Kiislamu iliyopewa jina la KCB Fursa Sukuk ilizinduliwa mnamo Novemba 9 na ilifungwa mnamo Desemba 5. Mfumo wa kifedha wa Kiislamu umestawi kwa kasi barani Afrika katika miaka ya hivi karimu.

4125709

captcha