IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Jarida chafu la ufuska Ufaransa lina uhsama na Uislamu

18:21 - January 13, 2023
Habari ID: 3476396
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran, ameashiria hatua ya jarida moja la Ufaransa kumvunjia heshima Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: Maadui wanataka kuzima nuru ya Uislamu lakini kwa neema ya Mwenyezi Mungu na nuru hii haiwezi kuzimwa kwa na ni wazi kuwa mzizi wa matusi haya ni uadui dhidi ya Uislamu.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa: “Jarida hilo chafu la ufuska limezitusi itikadi za mamilioni ya Waislamu kwa kumvunjia heshima Marjaa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.”

Inafaa kuashiria hapa kuwa, katika toleo lake maalumu la Jumatano ya tarehe 4 Januari, jarida la Charlie Hebdo Ufaransa lilifanya kitendo hicho cha kifidhuli kupitia uanzishaji wa shindano la kimataifa la michoro na vibonzo, ambapo lilichapisha picha za uvunjiaji mkubwa wa heshima zilizoandamana na maneno na misemo michafu na ya matusi dhidi ya viongozi wa dini.  Jarida hilo pia limewahi kuchapisha mara kadhaa vibonzo vyenye kumvunjia heshima Mtume Mtukufu Muhammad SAW.

Kwingineko katika hotuba yake, Ayatullah Khatami amesema  visiwa vitatu vitabaki kuwa vya Iran milele na hakuna mtu yeyote aliye na dhamira ya kuingiza mkono wake humo, kwani hataweza kufanya chochote, kama ambavyo hajaweza kufanya hivyo hadi sasa.

Ametoa msimamo huo kufuatia kauli za baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu zilizoko pembeni ya Ghuba ya Uajemi kuhusu visiwa vitatu vya Iran vya BuMusa, Tunb Kubwa na Tunb Ndogo na akasisitiza kwamba, visiwa hivyo ni milki ya Iran, kama ambavyo katika nyaraka za kale, njia ya majini ya Ghuba ya Uajemi imetajwa pia kwa jina lake hilo.

Kuhusiana na kuendelezwa vikwazo dhidi ya Iran, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema: Ulaya, Marekani na waitifaki wao wamejiwekea mashindano ya uwekaji vikwazo kwa lengo la kuitenga Iran lakini hawataweza katu kufikia lengo hilo.

Ayatullah Khatami ameashiria pia hatua ya bunge la Uingereza ya kuliwekea vikwazo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC na akasema: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Vikosi vya Ulinzi, jeshi la kujitolea la wananchi Basiji na Wizara ya Uinzi ni mihimili imara ya taifa la Iran; kwa hivyo kuiwekea vikwazo mihimili hiyo na kuitangaza kuwa ya kigaidi ni sawa na kuchukua msimamo dhidi ya taifa la Iran.

4114253

captcha