IQNA

Hujuma ya kigaidi

Iran yawakamata wahusika 6 wa hujuma ya kigaidi dhidi ya Haram Takatifu ya Shah Cheragh

22:33 - October 31, 2022
Habari ID: 3476015
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Intelijensia (Usalama) ya Iran imetangaza kuwa, imewatambua na kuwatia nguvuni watu sita katika timu ya usaidizi ya magaidi watenda jinai dhidi ya Haram takatifu ya Ahmad bin Musa (AS) maarufu kama Shah Cheragh huko katika mji wa Shiraz.

Watu 15 wakiwemo watoto wawili waliuliwa shahidi na wengine 30 kujeruhiwa baada ya gaidi mmoja kuwashambulia kwa risasi Jumatano iliyopita katika Haram takatifu la Ahmad bin Musa (AS) huko katika mji wa Shiraz makao makuu wa mkoa wa Farsi kusini mwa Iran. 

Gaidi wa kwanza aliyetekeleza hujuma hiyo tajwa alijeruhiwa kabla ya kukamatwa ambapo baadaye alipoteza maisha akiwa anapata matibabu hospitalini. Umoja wa Mataifa na nchi mbalimbali duniani zimelaani hujuma hiyo ya kigaidi huko Shiraz ambapo kundi la kitakfiri la Daesh limekiri kuhusika. 

Wizara ya Intelijensia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumatatu imetoa taarifa na kutangaza kuwa imefanikiwa kuwatambua na kuwatia mbaroni gaidi nambari mbili aliye na mkono katika oparesheni hiyo ya kigaidi pamoja na watu wengine sita katika timu ya usaidizi ya magaidi watenda jinai katika Haram takatifu ya Shah Cheragh, kwa kushirikiana na wananchi walio macho na makini wa Iran ya Kiislamu. Taarifa ya Wizara ya Intelijensia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza kuwa taarifa zaida kuhusiana na tukio hilo zitatangazwa hapo baadaye.  

4095930

Kishikizo: iran shah cheragh ugaidi
captcha