IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washiriki 400 waliohifadhi Qur’ani mashindano ya Qur’ani mjini Doha

21:21 - September 13, 2022
Habari ID: 3475774
TEHRAN (IQNA) – Mchujo wa duru ya 27 ya Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikh Jassim bin Mohammed bin Thani mwaka 2022 huko Doha, Qatar, imehudhuriwa na washindani wapatao 400.

Washindani ni raia na wakazi wakiwemo wanaume na wanawake.

Wanashiriki wanashindana katika kuhifadhi juzuu moja kati ya juzuu tano za mwisho za Qur’ani Tukufu.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya shindano hilo Jassim Abdullah Al Ali alisema kuwa takriban kamati 18 zinasimamia mitihani ya wanaume wanaoshindana katika Msikiti wa Imam Muhammad bin AbdulWahhab.

Kamati kumi na moja zinazosimamia zinaendesha mitihani kwa washindani wa kike katika makao makuu ya idara ya kuhifadhi Qur'ani ya wanawake katika eneo la Al Waab.

Alisema mitihani ya sehemu ya watoto itaendelea hadi Alhamisi, wakati mitihani ya makundi mengine itaanza Jumanne na kuendelea hadi Jumapili.

Kamati imetenga tuzo za fedha kwa washindi wa shindano hilo.

3480463

captcha