IQNA

Palestina

Maelfu ya Wapalestina wahudhuria Sala ya Fajr katika Msikiti wa Al-Aqsa

22:16 - September 09, 2022
Habari ID: 3475757
TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya Wapalestina waliswali Sala ya jamaa ya Fajr (alfajiri) katika Msikiti wa Al-Aqsa ulio kaitka mji unaokaliwa kwa mabavu na Israel wa al-Quds (Jerusalem) siku ya Ijumaa.

Waumini walikuja kutoka sehemu mbalimbali za Palestina na kukusanyika katika sehemu tofauti za eneo hilo  takatifu kwa ajili ya Sala ya Fajr asubuhi ya leo.

Hii ni sehemu ya kampeni iliyopewa jina la "Sauti ya Alfajiri Kuu" iliyoanzishwa na Wapalestina wakilalamikia hatua za utawala wa Israel dhidi ya maeneo matakatifu ya Waislamu huko Al-Quds na kwengineko katika ardhi za Palestina zinazokoloniwa na utawala huo dhalimu.

Katika kampeni hii, watu kutoka pande zote za Palestina wanakwenda Al-Quds kuswali swala ya Fajr kwenye Msikiti wa Al-Aqsa.

Vikosi vya utawala wa Israel na walowezi wa Kizayuni wamezidi kukiuka matukufu ya Msikiti wa Al-Aqsa katika miezi ya hivi karibuni.

Maafisa wa Israel wenye misimamo mikali na walowezi wa  Kizayuni mara kwa mara huvamia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa katika mji huo unaokaliwa kwa mabavu, hatua ya uchochezi inayowakasirisha Wapalestina.

Uchochezi huo hufanyika kwa amri ya makundi ya mahekalu yanayoungwa mkono na Tel Aviv na chini ya mwamvuli wa polisi wa Israel huko al-Quds.

Aidha, uchimbaji haramu wa Israel katika Msikiti wa Al-Aqsa umeharibu muundo wa msikiti huo.

Israel iliiteka Mashariki ya al-Quds, ulipo Msikiti wa Al-Aqsa, wakati wa Vita vya Siku Sita mwaka 1967 katika hatua ambayo haijawahi kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

4084260

captcha