IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu

Msikiti wateketezwa moto kwa makusudi magharibi mwa Ufaransa

23:27 - June 16, 2022
Habari ID: 3475384
TEHRAN (IQNA)-Mtu asiyejulikana ametekteza moto msikiti katika mji wa Rennes magharibi mwa Ufaransa na tayari mamlaka imeanzisha uchunguzi kuhusu jinai hiyo.

Tukio hilo lilishutumiwa vikali na wanaharakati wa mitandao ya kijamii. Picha zimesambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha moto ukiwa umefika maeneo yote ya msikiti kama sehemu huku wazima moto ikifanikiwa kuzima moto huo.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa polisi wamethibitisha kuwa moto huo umewashwa na mtu asiyefahamika alionekana akiwasha moto katika msikiti na hivyo tetesi kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu katika mfumo wa umeme zimetupiliwa mbali

Gazeti la Figaro liliripoti kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa René ilitangaza kuanza kwa uchunguzi wa tukio hilo. Gazeti hilo lilimnukuu Sheikh Mohammad Deco, imamu wa msikiti huo akisema hakuna mtu aliyekuwa ndani ya msikiti huo wakati wa moto huo.

Waislamu wengi waliokuja kusali walisikitishwa na uharibifu uliosababishwa na moto huo. Wanaharakati kwenye Twitter walikosoa namna vyombo vya habari vilivyopuuza jinai hiyo ya chuki dhidi ya Waislamu.

Tayari Waislamu wengi wameshatangaza nia ya kusaidia ukarabati wa msikiti huo.

Mnamo Aprili mwaka jana, kituo cha kitamaduni cha Kiislamu huko Rennes kilichafuliwa kwa maandishi yanayopinga Uislamu.

Hivi karibuni  katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu hali ya haki za binadamu duniani, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilikosoa rekodi ya haki za Ufaransa, hususan sera yake kuhusu Waisamu na wakimbizi.

Licha ya Ufaransa kuwa na idadi kubwa ya Waislamu miongoni mwa nchi za Ulaya lakini imeweka vizuizi vingi dhidi ya uhuru wa kuabudu kwa Waislamu wa nchi hiyo. Sheria hizo za serikali dhidi ya Waislamu zimechocheza hisia za chuki dhidi ya Waislamu nchini humo.

4064752/

captcha