IQNA

Mwamko wa Waislamu waliosahaulika Bahrain dhidi ya ufalme wa kidhalimu

17:56 - February 14, 2022
Habari ID: 3474930
TEHRAN (IQNA)- Februari 14, 2022 inasadifiana na kumbukumbu ya miaka 11 ya mwamko na vuguvugu la watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa Al Khalifa.

Mchambuzi wa mambo kutoka  Marekani, Graham Fuller ameangazia hali ya Waislamu wa Bahrain na kusema: "Waislamu wa Bahrain ni watu waliosahauliwa."  Mtazamo huu kuhusu Waislamu wa Bahrain umeonekana waziwazi katika miaka 11 iliyopita.

Watu wa Bahrain walianza maandamano yya kiraia dhidi ya utawala wa ukoo wa Al Khalifa mnamo Februari 14, 201 wakitaka mageuzi katika muundo wa utawala na madaraka. Jambo la ajabu kuhusu maandamano ya Bahrain ni kwamba, utawala wa Al-Khalifa uliwaomba msaada watawala wenzao wa ukoo wa Aal-Saud nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kuzima maandamano hayo, na mnamo Machi 14, mwezi mmoja tu baada ya kuanza kwa maandamano ya wananchi Bahrain, Saudia ilituma askari nchini humo kukandamiza maandamano hayo ya amani. Jamii ya kimataifa haijachukua hatua dhidi ya kitendo cha Saudi Arabia kutuma askari wake Bahrain na kuwakandamiza zaidi Waislamu wanaodhulumiwa nchini humo.

Kufuatia kutumwa askari kandamizi wa Saudia nchini Bahrain, kumeshuhudiwa mpasuko mkubwa baina ya  wananchi wataka mageuzi na utawala wa Al-Khalifa.  Ukoo unaotawala Bahrain wa Al-Khalifa unapinga mabadiliko yoyote nchini humo na kwa msingi huo unawakandamiza na kuwaua wananchi wanaotaka magaeuzi. Idadi kubwa ya waandamanaji wameuawa au kujeruhiwa huku wengine wengi wakikamatwa na kufikishwa katika mahakama za kijeshi na wananyimwa haki ya kujitetea. Wanaharakati wa mashirika ya kiraia na viongozi wa kidini ni miongoni mwa raia wanaofungwa jela muda mrefu nchini Bahrain na wengine pia wamebaidishwa.

Ukandamizaji huo usio na kifani haujawafanya wananchi wasitishe harakati zao bali maandamano yameongezeka na kuzidisha ufa baina ya ukoo wa Al-Khalifa na wananchi, na sasa nara na kauli mbiu ya wananchi imeguka kutoka matakwa ya mageuzi" na kuwa "mabadiliko" ya mfumo unaotawala.

Kadiri muda unavyosonga mbele, uingiliaji wa kigeni nchini Bahrain umeongezeka kiasi kwamba utawala wa Kizayuni wa Israeli unashirikiana na utawala wa Saudi Arabia katika kuusaidia utawala Al Khalifa kukandamiza mwamko na harakati ya kupigania mageuzi ya wananchi wa Bahrain. Utawala wa Al-Khalifa ambao kwa muda mrefu umekuwa na uhusiano wa siri na utawala wa Kizayuni wa Israel, ulitia saini makubaliano ya Abraham katika Ikulu ya White House mwezi Septemba 2020 katika fremu ya mpango wa rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump, ambapo kwa mujibu wa mapatano hayo, Bahrain imeanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina ukiwemo mji wa Quds (Jerusalem).

Hatua hiyo ya ukoo wa Al-Khalifa ilikabiliwa na maandamano makubwa ya wananchi wa Bahrain. Wananchi wa Bahrain wameeleza upinzani wao dhidi ya makubaliano hayo na kusema yana maana ya kuuhalalisha utawala wa kifalme wa Al Khalifa unaotaka kukandamiza zaidi mwamko wa wananchi kwa kuimarisha uhusiano na utawala haramu wa Israel. Huku maandamano yakiendelea kupinga kufunguliwa ubalozi wa utawala wa Bahrain mjini Tel Aviv, ubalozi wa Israel nchini Bahrain na vilevile kupinga safari za kidiplomasia kati ya Al Khalifa na utawala huo, hivi karibuni utawala wa Al Khalifa umeafiki afisa wa ngazi za juu wa jeshi la Israel atumwe nchini humo kwa ajili ya kazi rasmi.

Vyombo vya habari vya Kiebrania viliripoti kwamba, afisa mwandamizi wa jeshi la majini la utawala haramu wa Israel atapewa kazi Bahrain katika siku zijazo, ambapo pamoja na kushirikiana kwa karibu na vikosi vya usalama vya Manama, afisa huyo atakuwa na jukumu la kufanya mawasiliano na Kikosi cha Tano cha Jeshi la Marekani kilichoko Bahrain. Katika kujibu hatua hiyo ya Al Khalifa, kundi kubwa la upinzani la Jumuiya ya Kiislamu Al-Wefaq ambalo ni kundi kubwa zaidi la upinzani nchini Bahrain, limesema katika taarifa yake kwamba, kuteuliwa afisa wa jeshi la Israel huko Bahrain kunaashiria mporomoko wa kitaifa, kisiasa na uvamizi dhidi ya historia na mustakbali wa Bahrain, na kwamba ni  hujuma dhidi ya historia na mustakbali wa Bahrain mbali na kuwa ni uchokozi wa kiwango kikubwa dhidi ya Wabahraini unaotekelezwa na utawala wa Al-Khalifa.

Al-Wefaq aidha imesisitiza kuwa, hatua za utawala wa Al-Khalifa zimevuka mipaka na kwamba zimekiuka misingi ya kitaifa ya watu wa Bahrain. Imesema watawala wa ukoo wa Al Khalifa wanataka kuiuza nchi hiyo ili kupata madaraka ya kihaini, lakini walimwengu wanapaswa kujua kuwa serikali hiyo ya kifalme si halali na haiungwi mkono wa wananchi wa  Bahrain.

Nukta ya mwisho ni kwamba, vitendo hivi vinaashiria mpasuko kati ya Al Khalifa na watu wa Bahrain, na ni kilele cha mgogoro wa uhalali wa familia hiyo inayotawala Bahrain kwa mkono wa chuma.

4035870

Kishikizo: bahrain aal khalifa
captcha