IQNA

Mashindano ya Kuhifadhi Qur’ani nchini Kuwait

14:51 - August 27, 2021
Habari ID: 3474232
TEHRAN (IQNA)- Shirika la Wakfu la Kuwait limetangaza kuwa Duru ya 24 ya Mashindano ya Kitaifa ya Kusoma na Kuhifadhi Qur’ani Tukufu yanafanyika nchini humo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Wakfu la Kuwait Mansour Al Saqabi amesema lengo la mashindano hayo ni kuwahimiza vijana wa Kuwait kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu na watakaofanya vizuri katika mashindano hayo wataiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

Al Saqabi amesema nara na kauli mbiu ya mashindano hayo mwaka huu ni  اِطْمَئِنَّ (iṭmaʾinna) na yanafanyika chini ya usimamizi wa Emir wa Kuwait Sheikh Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ambaye ni kiongozi wa nchi hiyo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.

Ameongeza kuwa baada ya kufanyika mashindano ya mchujo katika maeneo mbali mbali ya nchi fainali zifafanyika katika Msikiti wa Jamia wa Kuwati mwezi Oktoba kwa muda wa wiki mbili na washindi watatangazwa.

3993106

captcha