Waziri Mkuu Sheikh Swabah al-Khalid al-Swabah alikutana na Amir Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Sabah, ambaye aliapishwa Jumatano. Waziri mkuu amejiuzulu kwa mujibu wa katiba ya nchi ili serikali mpya yenye mani ya amiri mpya ianze kazi.
Taarifa zinasema Sheikh Nawaf ametangaza kuwa na imani na baraza la mawaziri ambalo liliundwa Disemba.
Sheikh Nawaf, 83, alichukua mamlaka baada ya kufa ndugu yake aliyekuwa Amir, Sheikh Swabah, Jumanne iliyopita akiwa na umri wa miaka 91.
Wananchi wa Kuwait sasa wanasubiri kwa hamu kujua ni nani atakayeteuliwa na Sheikh Nawaf kuwa mrithi wa kiti cha ufalme ili amsaidie kuendesha nchi wakati huu bei ya mafuta imeporomoka kufuatia janga la corona na hivyo kuathiri vibaya uchumi wa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi. Atakayeteuliwa katika nafasi hiyo anapaswa kuidhinishwa na bunge.
3472747