IQNA

Katibu Mkuu wa zamani Jihad Islami aaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu

12:29 - June 07, 2020
Habari ID: 3472844
TEHRAN (IQNA) -Katibu Mkuu wa zamani Harakati ya Jihad Islami ya Palestina ameaga dunia hospitalini baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Taarifa iliyotolea na harakati hiyo imesema kuwa, Ramadhan Abdallah Shalah ameaga dunia akiwa hospitalini katika mji wa Gaza. 

Taarifa hiyo imeseama: Tumekuwa tukishuhudia mapambano ya Harakati ya Jihad Islami tangu kuanzishwa kwake, na tunakumbuka uongozi na msimamo wake wa kitaifa kwa heshima na fahari."

Imeongeza kuwa Shalah alilinda utambulisho wake wa Kiarabu na Kiislamu kwa kuunga mkono mapambano ya Palestina. 

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas pia ametoa ujumbe akieleza kusikitishwa na kifo cha Katibu Mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihadi Islami ya Palestina. 

Mahmoud Abbas amesema: "Palestina imempoteza shakhsia mkubwa wa kitaifa kwa kifo cha Ramadhani Shalah.

Mwaka 1991 hadi 1995 Shalah alikuwa mhadhiri wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Tampa, Florida nchini Marekani. 

Shalah ambaye alikuwa mtaalamu wa uchimi alizaliwa Ukanda wa Gaza mwaka 1958 na akateuliwa kuwa kiongozi wa Harakati ya Jihad Islami (Islamic Jihad Movement) mwaka 1995 baada ya mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Israel dhidi ya kiongozi wa kabla yake, Fathi Shaqaqi.

Mwaka 2003 Marekani iliweka jina la Dakta Ramadhan Shalah katika orodha yake ya magaidi kutokana na mapambano yake makali dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na mwaka 2017 Idara ya Upelelezi ya Polisi ya Federali ya Marekani (FBI) ilimuweka katika orodha ya watu wanaosokwa kwa udi na uvumba. 

Mwaka 2018 Ziad al-Nakhala aliteuliwa kuwa kiongozi mpya wa Harakati ya Jihad Islami baada ya Dakta Ramadhan Shalah kuzidiwa na maradhi.  

3471615

captcha